NA VICTORIA GODFREY

CHAMA cha Soka Wilaya ya Ilala (IDFA) kimepanga kuendesha ligi ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15(U15) mwezi huu.

Akizungumza na Zanzibarleo Katibu Mkuu wa IDFA Daud Kanuti,alisema maandalizi yanaendelea kuhakikisha inafanyika kwa weledi na ushindani.

Alisema tayari timu tano zilikuwa zimethibitisha kushiriki ligi hiyo kabla ya kutangaza kwa maombolezo.

” Tunatarajia timu zitajitokeza kwa wingi kuthibitisha, na hii ni kwa ajili ya maendeleo ya mpira ndani ya wilaya na kutoa fursa kwa vijana kuonyesha vipaji,” alisema Kanuti.

Alizitaja timu zilizothibitisha hadi sasa ni EFCA, Kimanga United,Eleven Kids,Global Winners na Kisa.