TRIPOL, LIBYA

WAZIRI Mkuu wa Libya Abdul Hamid Dbeibah, amekutana na waziri mkuu mwenzake wa Italia, Mario Draghi, katika mji mkuu wa Tripoli na kujadili ushirikiano baina ya nchi mbili hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya habari ya serikali, Libya imesifu uungaji mkono wa Italia kuhusu mzozo wa nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, ambapo Dbeibah alisema Libya iko tayari kujenga ushirikiano wa kimkakati na Italia.

Pamoja na mambo mengine lakini viongozi hao wawili walisema kuwa wanaangalia kujenga uhusiano wao mpya ili kukuza ushirikiano wa nchi mbili, makubaliano hayo ni pamoja na kufungua upya safari za anga ya Italia ili kuruhusu ndege ndege za Libya.

Waziri mkuu wa Libya pia alisema Libya na Italia zinakabiliwa na changamoto ya pamoja ya uhamiaji haramu, ambao unahitaji mchango kutoka kwa jamii ya kimataifa.

Draghi aliangazia umuhimu wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika maeneo ya miundombinu, nishati, na huduma za afya, akisifu juhudi za Libya kwa kupambana na uhamiaji haramu.