D’JAMENA, CHAD

MATAIFA mbalimbali duniani pamoja na jumuiya za kimataifa zimelaani mauji ya Rais wa Chad yaliyofanywa na waasi hapo juzi.

Rais wa Cameroun Paul Biya ambayo ni nchi jirani na Chad, hapo Jumanne alituma salamu zake za rambirambi juu ya kifo cha Rais wa Chad Idriss Deby.

“Ningependa kutoa salamu zangu za pole na dhati kwa taifa lililofiwa la Chad,” Biya alisema katika taarifa iliyochapishwa na Twitter.

Ilikuwa ni “hasara kubwa” kwa Chad, eneo ndogo la Afrika ya Kati, na bara la Afrika, Biya aliongeza katika taarifa hiyo kwa Mahamat Deby, mtoto wa rais wa zamani. Mahamat ataongoza baraza la kijeshi la mpito kwa miezi 18 baada ya kifo cha baba yake.

Nae Mkuu wa Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, ambae aliwahi kuwa waziri mkuu wa zamani wa Chad, alisema amesikitishwa sana na kifo cha Deby, na alituma salamu za pole kwa familia yake.

Nayo Ufaransa ambayo ni koloni la Chad, imelaani mauji ya Rais Deby na kusema kuwa jeshi ni lazima lichukue hatamu na pia likihimiza kurudi haraka kwa utawala wa raia na mabadiliko kwa amani.

“Ufaransa imepoteza rafiki shujaa,” ofisi ya Rais Emmanuel Macron ilisema katika taarifa. “Inaelezea kushikamana na wachad wote katika kipindi cha majonzi”, ilisema taariufa na kutaka utulivu na uadilifu nchini humo.

Nao Umoja wa Ulaya kupitia Mkuu wa maswala ya kigeni wa Jumuiya hiyo, Josep Borrell, alielezea rambirambi zake kwa familia, na kwa mamlaka ya Chad na watu wake.

“EU inatoa wito kwa wahusika wote kuchukua hatua stahiki sambamba na kudumisha amani na utulivu”, alisema Borrell.

Wakati huo huo, Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel alisema kuwa “utulivu, usalama na uadilifu nchini Chad kwa sasa unahitajika.

Kwa upande wake Umoja wa Mataifa chini ya Volkan Bozkir, rais wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, alituma salamu za rambirambi kwa Chad na alisema kuwa ni pigo kwa serikali ya Chad na watu wake.

Nayo Mali ambayo ni nchi jirani na Chad limesema utawala wa kijeshi wa mpito ni jambo linalotazamiwa kwa sasa, alisema Bah Ndaw na kuonyesha  “huzuni kubwa” juu ya habari ya “kifo cha kinyama” cha Deby.

Aidha Niger Katika taarifa rasmi, Rais Mohamed Bazoum na serikali katika nchi jirani ya Niger walisikitishwa na kifo cha Rais Deby na kusema nchi hiyo inaungana na chad katika kipindi hiki cha msiba.

Taarifa hiyo pia iliwahakikishia watu wa Chad juu ya “kujitolea kufanya kazi pamoja nao kwa amani na utulivu na Nchi za G5 Sahel na Mataifa yanayopakana na Ziwa Chad”.

Kwa upande wake Senegal chini ya rais wake Macky Sall alisema anauheshimu  mchango wa rais Deby. Nayo Israeli chini ya waziri Mkuu Benjamin Netanyahu aliwasilisha salamu za rambirambi kwenye Twitter, akisifu “uongozi wa ujasiri na … uamuzi wake wa kihistoria kwa kufanya upya uhusiano wa Chad na Israeli”.

Rais Deby alikufa Jumanne kutokana na majeraha aliyoyapata katika mstari wa mbele wa vita dhidi ya waasi, kulingana na taarifa iliyosomwa kwenye runinga ya kitaifa na msemaji wa jeshi la Chad, Jenerali Azem Bermandoa Agouna