NA NASRA MANZI
TIMU ya Kahawa Veterani SC imefanikiwa kutinga hatua ya nusu finali baada ya kuifunga timu ya Mtumbani Veterani mabao 2-1
Mchezo huo wa robo fainali ya ligi ya mashindano ya Dulla Sunday uliochezwa wakati wa jioni kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
Katika mtanange huo Mtumbani Veterani walikuwa wa kwanza kuona lango la wapinzani wao lilowekwa wavuni na Jabir Salum dakika ya 25, bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kurudi tena kipindi cha pili kumalizia hatua ya mwisho wanaume hao walishambuliana kwa kila timu kutaka kuondoka na pointi tatu.
Katika mchezo huo dakika ya 46 timu ya Kahawa Veterani ilisawazisha bao lilowekwa kimiani na mshambuliaji Omar Bakari,
Wakati bao la pili lilifungwa na Mshenga Kombo katika dakika ya 53 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Othman Juma.
Kwa matokeo hayo timu ya Kahawa Veterani itashuka dimbani Ijumaa kuvaana na Real Zanzibar kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.