NA ASIA MWALIM
JESHI la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, limewakamata watu 315 wanaokabiliwa na tuhuma mbali mbali, pikipiki 13 zikiwemo tatu kutoka Tanzania bara zilizovushwa katika bandari bubu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, ACP Awadh Juma Haji, aliyasema hayo alipokua akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Mwembemadema Zanzibar.
Kamanda Awadh, alisema watu hao pamoja na vyombo hivyo vilikamatwa katika operesheni waliyoiendesha ndani ya miezi mitatu kwa mwaka huu, katika maeneo mbali mbali katika Mkoa wa Mjini.
Akifafanua taarifa hiyo alisema, alieleza kuwa pikipiki 13 zilikamatwa katika operesheni hiyo ambapo pikipiki tatu ziliripotiwa katika vituo vya polisi kuibiwa katika maeneo ya Mkoa wa Mjini Magharibi pamoja na watuhumiwa waliohusika na wizi huo.
Akitaja pikipiki tatu zilizoibiwa ni aina ya Vario rangi nyeupe yenye namba za usajili Z. 241 LH, pikipiki aina ya boxer rangi nyeusi yenye namba za usajili Z.698 LB na pikipiki aina ya vario rangi nyeupe yenye namba za usajili Z. 231 HZ.
Pikipiki nyengine alisema ziliibiwa katika mikoa ya Tanzania bara na kuletwa Zanzibar kupitia bandari bubu, lakini jeshi hilo ilizikamata pamoja na mtuhumiwa mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Ali Ubwa Hassan (27) mkaazi wa Bububu.
Alitaja namba za pikipiki hizo, alisema ni MC 690 CTZ cheses namba MD 625 AF49 MIAA5120 aina ya Boxer bajaji rangi ya blue, Cheses namba MD2B15BX8LWJ89117aina ya Boxer bajaji rangi nyeusi na Cheses namba MD2B15BX8LLC94957 aina ya Boxer bajaji rangi nyeusi.
Vile vile, Kamanda huyo alisema pikipiki tano zilitelekezwa maeneo mbalimbli ndani ya Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya wahusika kuwaona askari waliokua doria kukimbia, jambo ambalo linaonesha ni dalili kuwa pikipiki hizo zitakuwa ni za wizi.
Akizitaja alisema ni Vespa rangi nyekundu yenye namba za usajili Z. 563 DL , SANLG rangi nyekundu yenye namba za usajili Z. 807 KM, Watco rangi nyeusi, Z.774 KS na nyengine ni pikipiki aina ya Vespa rangi ya buluu ambayo haina namba za usajili, ilitelekezwa maeneo ya Mtoni kwa Kisasi ambapo namba zake hazisomeki vizuri.
Kamanda alisema pikipiki moja aina ya Watco yenye rangi nyekundu isiyo na namba za usajili na namba za pikipiki hiyo zinatia shaka kwani hazisomeki vizuri.
Aidha pikipiki mpja aina ya Vespa rangi nyeusi yenye namba za usajili Z. 259 KV ambayo ilikutwa ikiwa na bangi kilogramu 2.33 iliyokuwa imewekwa katika buti ya Vespa hiyo.
Ambapo katika operesheni hizo wamefanikiwa kuikamata gari moja yenye namba za usajili Z.179 JD aina ya Alphard rangi ya silver.
Alisema kuna watu wengi ambao wamewahi kuibiwa vyombo vya usafiri wa maringi mawili na kuvikosa, hivyo wafike vituo hivyo ili kukagua na kuhakikisha ikiwa ni vyao.
Kamanda huyo amewataka wananchi waliowahi kuibiwa vyombo vya maringi mawili kufika kituo cha Polisi Madema, Mazizini, Bububu ili kuvitambua vyombo hivyo.
Katika hatua nyengine Jeshi la polisi Mkoa wa mjini Magharibi Unguja limefanikiwa kukamata watuhumiwa 315 wanaohusika na makosa tofauti ikiwemo pombe haramu aina ya gongo, usafirishaji kwa njia ya magendo, wizi, unyanganyi kuvunja na kuiba, ambapo kati yao wanaume ni 292 na wanawake 23.
Hivyo watuhumiwa waliokamatwa kwa kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi 23 wote wa kiume, waliopatikana na pombe aina ya gongo ni wanane na watuhumiwa 284 wamepatikana na makosa mengine.
Aidha vitu vyengine vilivyokamatwa ni dawa za kulevya aina ya bangi kilo 38.25, pombe aina ya gongo lita 35, mtambo wa kutengenezea pombe za kienyeji, pikipiki 13 ndoo 4 za rangi zenye ujazo wa lita 20 kila moja.