NAIROBI, KENYA
RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewafukuza kazi wakurugenzi wote wa bodi ya wakala wa usambazaji wa dawa nchini humo.
Hatua hii imekuja baada ya KEMSA kukabiliwa na kashfa kadhaa miaka ya hivi karibuni ikiwemo ya vifaa vya kujikinga na covid-19, huku usambazaji wa dawa ukiainishwa kuwa miongoni mwa sababu zilizosababisha.
Kashfa ya hivi karibuni ilihusisha dozi 24,000 za dawa za kupunguza makali ya UKIMWI ambazo tayari zimeondolewa kwa ajili ya matumizi.
Kenya imesitisha matumizi ya Nevirapine mwaka 2019 baada ya wagonjwa kuanza kuathirika na dawa hizo.
Wakala hao ni sehemu ya sababu ya kwanini zaidi ya dozi 200,000 za dawa ya anti-retroviral zimekwama katika ghala iliyopo Mombasa, miezi minne baada ya US-AID kutoa msaada.
Mwaka jana, KEMSA ilishutumiwa kutumia vibaya mamilioni ya dola kununua vifaa kinga vya Covid-19.
Hata hivyo wakala hao wanatarajiwa kurudisha imani kwa umma.Na Bodi mpya inatarajiwa kuanza kazi wiki tatu zijazo.