JUBA, SUDAN KUSINI
RAIS wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit amerejea nchini humo baada ya kumaliza ziara ya siku tatu nchini Afrika Kusini, ambapo akiwa huko alikutana na ufanya mazungumzo na rais wa nchi, Cyril Ramaphosa.
Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini, Dk. Naledi Pandor, ambapo katika mazungumzo yao, rais Ramaphosa alihimiza kutekelezwa kwa mkataba wa makubaliano baina ya serikali ya nchi hiyo na upinzani.
Alisema hali ya usalama nchini humo itarejea endapo mkataba huo utatekelezwa na pande zote mbili na hakuna kuwa na wasiwasi wa vita ambavyo vinawaathiri sana wananchi wa taifa hilo.
Aidha waziri huyo alisema mbalimbali viongozi hao kuzungumzia umuhumi wa kuheshimiwa mkataba wa amani, pia alizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi zao.
Kwa mujibu wa gazeti la Post linalochapishwa nchini Sudan Kusini kiongozi huyo akiwa katika kiwanja cha ndege cha Juba hakufafanua kwa undani maeneo ya ushirikiano waliyozungumza kati yake na Ramaphosa.
Rais huyo aliondoka nchini humo Aprili 15 mwaka huu, ambapo katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha mjini Juba, rais Kiir alisema ziara yake imekuwa ya mafanikio nchini Afrika Kusini.