NA MWANAJUMA MMANGA

TAASISI ya Utafiti wa Uvuvi na Mazao Baharini, imeanza utekelezaji  wa sera ya uchumi wa bluu na uvuvi kwa lengo la kuwasaidia wananachi kutumia fursa zilizomo katika sekta hiyo.

Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa taasisi hiyo Ramla Omar, aliyasema hayo baada ya uzinduzi  wa uvunaji wa majongoo ya bahari katika shehiya ya Kikungwi na kueleza kuwa ufugaji wa majongoo baharini wafugaji wanaweza kufuga kibiashara zaidi.

Alisema iwapo wafugaji hao watafuga kibiashara wataweza kujikwamuna na hali ngumu za kimaisha na kupata kipato cha mtu mmoja na serikali kwa ujumla.

“Wafugaji watajikita zaidi kufuga kibiashara wataweza kupata tija zaidi na kupunguza tatizo la ajira kwa wananchi na kufaidika na fursa hiyo katika kujikwamua na umaskini nchini” alisema.

Alisema eneo la Kikungwi lilikuwa limefungwa kwa kipindi kifupi cha mwezi mmoja na wiki mbili kwa shughuli ya ufugaji majongoo kwa ajili ya majaribio ya utafiti na kufunga eneo la Bungi na Kikungwi kwa shughuli hiyo.

Alisema utafiti huo umefanyika 2019 kwa kulifunga eneo hilo kwa shughuli hiyo kwa ajili ya upatikanaji wa vifaranga vya majongoo ambao utafiti ulionesha maeneo 18 yalijitokeza Zanzibar na manane kwa Pemba ambapo  Bungi na Kikungwi yameonekana ni mazuri kwa ufugaji wa majongoo.

Alisema walifunga maeneo hayo, Januari 15, 2021 na pia walikuwa wanafatilia kwa ukaribu ukuaji pamoja na maendeelo ya ufugaji wa majongoo hayo kwa kutumia taaluma ili kupata vifaranga zaidi ya 100,000.

Alisema wataendeela kufunga maeneo hayo kwa ajili ya kufuga vifaranga kwa ajili ya kuwapatia wananchi, kwani  taasisi ya utafiti inafanya kazi kwa mashirikiano na Idara ya Maendeelo ya Uvuvi kwa pamoja ili kuona wanawasaidia wanaachi wanaoishi karibu na pwani.

Nae Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Said Juma Ali, alisema upatikanaji wa majongoo bahari katika pwani ya shehiya Kikungwi kutasidia kupunguza  changamoto ya uhaba wa vifaranga vya majongoo kwa wafugaji nchini.

Aliyasema hayo katika uzinduzi wa uvunaji wa majongoo ya bahari katika shehiya ya Kikungwi mpango ambao  unatekelezwa kwa kushirikiana na uchumi wa bluu na sio kazi rahisi kama inavyopangwa na ni lazima kufanywe utafiti.

Alisema lengo la mradi huo ni kujikomboa wananchi wa kijiji hicho kimaisha katika maeneo ambayo wanatayojishughulisha uvuvi wa baharini, kwani kila mwezi wanapata tani 300 ya ufugaji wa majongoo katika shehiya hiyo.

Ofisa Maendeelo ya Uvuvi Kitengo cha Ufugaji wa Mazao ya Baharini, Tomas Rafael, alisema zoezi la kuhifadhi Majongoo limeanza tangu Januari na wananachi wa Kikungwi wamelifurahiya kwani wamekuwa  ubunifu wazuri

Alisema wananchi wa kijiji hicho wanajivunia kupata majongoo mengi muda wa usiku na wamepata mafanikio makubwa, hivyo wameshauri kuongeza maeneo mengine ya kufugia ikiwemo Ukanga na maeneo mengine mazuri kwa hifadhi kwani ni faida kwao na jamii kwa ujumla.

Alisema takriba kuna kampuni nne zimejitokeza kununua majongoo hayo  kwa ajili ya kuendeleza kuwafuga na kufanya biashra , ambapo kampuni hizo ni Ocean, Sun raice, wakulima hai na N Z wanafuga mashamba mbali mbali ikiwemo Fukuchani na maeneo mengine.

Katibu wa Kamati ya Uvuvi shehiya ya Kikungwi, Bahati Issa Suleiman, amesema wanafaidika kilimo cha majongoo kwa asilimia kubwa sana na ni faraja kubwa na katika maeneo yanayoingia jongoo jingi ni shehiya ya Kikungwi.

Alisema wanawake wanafaidiak mara mbili zaidi ikiwemo kujiajiri na kuondokana na utegemezi.

Kwa upande wake Sheha wa Kikungwi, Mohammed Haji Shahidi, wameishukuru Idara na serikali kwa ujumla kuwasaidia wananachi wa Kikungwi na kushukuru wananchi kukubali na ameiomba kuwapelekea wataalamu na kuwapatia vifaa.