JARKATA, INDONESIA

IDADI ya watu waliokufa kwa kimbunga cha Seroja nchini Indonesia katika mkoa Nusa Tenggara mashariki mwa nchi hiyo imeongezeka na kufikia 124 huku wengine 74 hawajulikani walipo.

Kwa mujibu wa msemaji wa mamlaka ya taifa ya kukabiliana na maafa nchini humo, Raditya Jati, alisema vifo hivyo vilivyoripotiwa katika wilaya za Mashariki mwa mkoa wa Nusa Tenggara, Lembata, Malaka, Sabu Raijua, Ende na Kupang na Kupang jiji moja.

“Takwimu hii bado ni ndogo ukilinganisha na janga lilivo huku juhudi za mchakato wa uokoaji bado unaendelea,” Jati aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

Sambamba na hilo, watu 129 walijeruhiwa huku watu 13,230 wakihama makaazi yao katika sehemu kadhaa za uokoaji, na vituo 87 vya umma viliharibiwa.

Jumla ya nyumba 688 ziliharibika vibaya huku 272 zikiwa zinakalika na nyumba 154 zikiwa zimepata athari ndogo tu.

Wakati huo huo, maeneo kadhaa bado yamefungwa kutokana na kuanguka kwa nguzo za umeme huku mamlaka zikisambaza vyakula, blanketi na mahema kwa waliokimbia makazi yao.

Mamlaka ya hali yahewa nchini homo ilisema kuwa mvua kubwa, upepo mkali, na mawimbi ya bahari ya juu hadi mita sita yalitokea baada ya kimbunga cha Seroja kupiga katika Bahari ya Savu, kusini mwa mkoa wa Nusa Tenggara Mashariki.

Seroja ni kimbunga cha msimu wa mwaka ambapo kilipiga takriban miaka 10 iliyopita yaani mwaka 2008.