NA ZAINAB ATUPAE
KLABU ya KMKM inayoshiriki ligi kuu ya Zanzibar imeondoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kianga International inayoshiki ligi daraja la pili Wilaya ya Magharibi A ikiwani ni muendelezo wa mchezo wa kirafiki.
Mchezo huo uliotimua vumbi uwanja wa Kianga majira ya saa 10:00 jioni uliokuwa wa ushindani kwa timu zote mbili.
Hadi timu hizo zinatoka uwanjani kupata mapumziko KMKM ilikuwa ikiongoza kwa mabao mawili.
Mabao hayo yalifungwa na Mohamed Said ‘Mesi dakika ya 23 na bao la pili liliongezwa na Salim Akida dakika ya 34.
Kurudi uwanjani kumalizia kipindi cha pili timu hizo zilingia na kasi kubwa na kufanya mabadiliko ya wachezaji kulingana na makosa yao.
Lakini dakika 45 za kipindi cha pili zinamalizika hakuna timu iliongiza bao ambapo KMKM ilifanikiwa kubakiwa na mabao yake mawili,huku Kianga International ikitoka bila ya bao.