NA ZAINAB ATUPAE

BENCHI la ufundi la timu ya kuzuia magendo KMKM limesema wanamategemeo makubwa ya kuanza mazoezi mwezi 20 Ramadhani.

Akizungumza na Zanzibar leo kocha mkuu wa timu hiyo Ame Msim, alisema awali walitarajia kuanza mazoezi mwezi 15 Ramadhani, lakini kutokana wamelazimika kusogeza mbele.

“Ni kweli mwanzo tulisema tutaanza mwezi 15, lakini haikuwezekana na tunatarajia kuanza mwezi 20”,alisema.

“Kucheza mechi na timu ambazo zinatafuta nafasi ya kuzuia daraja ni kazi sana na pia ni ngumu kushinda, kwani nazo zinatafuta ushindi,ili kupata pointi zitakazo wasaidia kutoshuka daraja,”alisema.

Alizitaja mechi zilizobaki dhidi ya Chuoni ,Polisi,Black Sailors na KVZ ambapo kati ya hizo mbili zinatafuta nafasi ya kutoshuka daraja na mbili zinataka nafasi mbili za juu.

“Chuoni na Polisi zipo katika hali mbaya  kwenye msimamo wa ligi na zinahitajia kushinda mechi zote zilizobakia,”alisema.

KMKM inaongoza ligi kuu ya Zanzibar ikiwa na pointi 36, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Mafunzo yenye pointi 33 na nafasi ya tatu KVZ pointi 31.