NA FATUMA KITIMA,DAR ES SALAAM

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika swala ya Idd Fitri, ambayo kitaifa itasaliwa katika Uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungunza na Zanzibar Leo jana, Sheikh wa Mkoa wa Dae es Salaam, Alhad Mussa Salum, amesema sikukuu inaweza kuwa Mei 13 mwaka au Mei 14, italingana na mwezi utakavyoandama.

Sheikh Alhad alisema mara baada ya kukamilika sala hiyo litafuatiwa na Baraza la Idd, litalofanyika katika viwanja vya Karimjee, hivyo aliwaomba waumini wa dini ya kiislam kuhudhuria kwa wingi siku hiyo.

Alisema waumini wa dini ya kiislam ni vyema wakatumia siku hiyo kwenda katika mabaraza, ili kusikiliza mawaidha mbali mbali, ili kuendelea kumtukuza Mwenyezi Mungu .

Aidha alieleza hakuna budi kwa waumini wote dini ya kiislam kuendelea kumcha Mwenyezi Mungu na kufuata yale mema aliyoyamrisha na kuacha yaliyokatazwa.