NAIROBI, KENYA
WANAJESHI wa Kenya watajiunga na kikosi cha FIB (Force Intervention Brigade) Mashariki mwa DRC ili kulisadia jeshi la nchi hiyo kukabiliana na makundi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo.
Hatua hiyo imefikiwa kutokana na makubaliano baina ya rais wa DRC Felix Tshisekedi wakati alipokutana na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alipokuwa ziarani nchini DRC.
Viongozi katika moja ya mambo waliyokubaliana ni kusaidia kukuza usalama mashariki mwa DRC ambapo Kenya itatuma kikosi cha wanajeshi kusaidiana na jeshi la DRC katika hatua zake za kiyafyeka makundi ya waasi.
Sekta nyengine viongozi hao walizokubaliana kushirikana pamoja ni uchumi kilimo, elimu, afya, michezo na utalii. Nyingine ni mazingira, biashara za ndogo na za kadri, makazi, nishati na maendeleo ya miundombinu.
Aidha rais Tshisekedi na Kenyatta wametiliana saini mikataba miwili baina ya nchi hizo juu ya usalama na ulinzi ambayo hutoa mifumo ya ushirikiano kati ya Kenya na DR Congo katika maeneo kama vile ugaidi, uhamiaji, usalama wa mtandao, na forodha na udhibiti wa mipaka.
Makubaliano yaliyofufuliwa juu ya usafirishaji wa baharini yanalenga kuiweka tena bandari ya Mombasa kama lango kuu la kuingia DR Congo kwa kurahisisha usafirishaji wa bidhaa hadi nchini humo