NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM
MWEKEZAJI na mdau wa Tasnia ya Habari na Burudani, Francis Ciza maarufu Majizo amewataka wasanii vijana kutokata tamaa kwenye kufikia malengo yao.
Majizzo ni mmiliki radio ya E-FM na TV ya E-TV, ambaye pia ni mume wa muigizaji Bongo Movie, Elizabeth Michael.
Akizungumza kupitia kipindi cha Joto la Asubuhi, Majjizo alisema dunia ya sasa inahitaji ushindani mkubwa sana katika kuhakikisha mafanikio makubwa yanafikiwa nasio kuishia njiani kama watu wengi wanavyofanya.
Alisema wasanii vijana wanapaswa kujituma kwa ufanisi mkubwa ili kupiga hatua nakufikia malengo yao ambayo wamejiwekea.
“Kwa sasa hapa nchini ushindani wa Sanaa umekuwa mkubwa hivyo jambo zuri vijana kujituma na kupambana ili kufikia malengo’’alisema..
“Kikubwa vijana wenzangu wanatakiwa kujua ili tufanikiwe ni lazima kujituma kwa ufanisi bila kukata tamaa,”alisema