LONDON,England

TIMU ya Manchester United imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Brighton &Hove Albion kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford.

Danny Welbeck alianza kuwafungia Brighton dakika ya 13, kabla ya Marcus Rashford kuisawazishia United dakika ya 62 na Mason Greenwood kufunga la ushindi dakika ya 83.

Kwa ushindi huo, Man United inafikisha pointi 60 baada ya kucheza mechi 30, ingawa inabaki nafasi ya pili sasa ikizidiwa pointi 14 na mahasimu wao wa Jiji, Manchester City ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi.