NA VICTORIA GODFREY

UONGOZI wa Shirikisho la Mieleka ya Ridhaa Tanzania (TAWF) umesema maandalizi ya mashindano ya Muungano yanaendelea vizuri.

Mashindano hayo yamepangwa kufanyika kuanzia Aprili 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Zanzibarleo,Katibu Mkuu wa TAWF Abraham Nkabuka,alisema bado wanahitaji wadau wa kusaidia kufanikisha hilo.

Alisema lengo ni kuungana na watanzania katika kuadhimisha sikukuu ya Muungano kupitia michezo pamoja na kutoa nafasi kuwa vijana kushiriki mashindano mbalimbali.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na tunaimani kuwa timu zitakuwa zimejiandaa na kujiweka tayari kwa ligi yetu na tutapata kike tulichokusudia,” alisema Nkabuka.

Alisema milango bado ipo wazi kwa timu na mchezaji binafsi kujitokeza kushiriki mashindano hayo ili kuonyesha viwango vyao na kuutangaza mchezo huo.