NA HASHIM KASSIM

MWENYEKITI wa Chama cha Mchezo wa ‘Taekwondo’ Zanzibar Maxmiliam Kailangana, amesema mchezo huo haukuletwa kwa kumdhuru mtu lakini upo kwa ajili ya kujilinda na kujenga nidhamu.

Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na gazeti hili, alisema kuna baadhi ya watu wanadhani mchezo huo ni kwa ajili ya ugomvi au kumdhuru mtu mwengine asiye na hatia.

Max aliongezea kuwa mchezo huo wa Taekwondo ni sanaa ambayo haifundishi kumdhuru mtu bali inafundisha nidhamu na ukakamavu.

“Mchezo huu ni sanaa ambayo haifundishi kumdhuru mtu bali inafundisha nidhamu na ukakamavu, lakini yote hii haimainishi kama sisi tunapiga watu ni michezo kama ilivyo mingine” alisema Max.

Vile vile akagusia suala la kuruka katika mchezo huo na kusema kwamba hiyo ni jadi ya mchezo wenyewe kwani asili yake ni Korea ambako watu walitumia kama sehemu ya kujilinda na ndivyo ilivyo na kwao pia.

Mwenyekiti huyo amesisitiza kuwa lengo la mchezo huo ni ulinzi binafsi yaani “self defense” na kuwataka watu kujiunga nao ambapo maskani yake Amani katika uwanja wa Judo.