NA JOSEPH DAVID

MENEJA wa mshambuliaji wa kimataifa wa Simba na nyota wa timu ya Taifa ya Rwanda Meddie Kagere, Patrick Gakumba ‘Super Manager’, ametamba kuwa uwezo wa mchezaji wake kufumania nyavu bado upo juu.

Akizungumza kwa njia ya simu kupitia kipindi cha michezo kutoka kituo cha Clouds Fm mara baada ya mechi ya Simba na Mtibwa Sugar wiki iliyopita, Gakumba alibainisha kuwa uwezo wa Kagere anaujua hivyo kutokufunga mechi kadhaa zilizopita ulikuwa ni upepo wa muda mfupi tu, hali ambayo inaweza ikamtokea mchezaji yeyote.

“Waliokuwa wanambeza Kagere leo amewazodoa kwa kuweka nyavuni mabao mawili,  hali kama hii iliwahi kumtokea hata msimu uliopita lakini mwisho wa msimu akaibuka kuwa mfungaji bora wa ligi,”alisema Gagumba.