VIONGOZI wa mataifa ya kadhaa ya kiarabu na yaliyo na waislamu wengi wamejitokeza hadharani kumuunga mkono Mfalme Abdallah II wa Jordan kufuatia mtikisiko wa hali ya usalama uliohofiwa kuwa jaribio la mapinduzi katika taifa hilo la mashariki ya kati.

Nchi jirani ya Saudi Arabia ilisema kwamba inauunga mkono kikamilifu utawala wa kihashimiyyah wa Jordan na pia hatua zilizochukuliwa na mfalme w ataifa hilo Abdullah wa pili na mrithi wa kiti cha Ufalme Hussein ili kulinda usalama na utulivu.

Taarifa kama hiyo imetolewa na katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, ambaye kupitia ukurasa wa Facebook, alisema jumuiya hiyo inaunga mkono moja kwa moja hatua zote za kudumisha usalama na utulivu.

Baraza la ushirikiano wa mataifa ya Ghuba (GCC) nalo pia limethibitisha kuunga kwake maamuzi yote ya utawala wa Jordan.

Hatua za nchi za kiarabu kuwamuunga mkono mtawala huyo wa Jordan imekuja kufuatia asubuhi ya Machi 4 mwaka huu  vyombo rasmi vya habari nchini Jordan vilionya kwamba usalama na utulivu wa nchi hiyo ni “mpaka usiopaswa kuchupwa.

Vyombo hivyo vimetoa onto hilo kufuatiwa kuwepo taarifa kwamba mwanamfalme Hamzah kuhusishwa na njama za mapinduzi kutaka kumpindua kaka yake mfame wa Abdullah wa Jordan.

Baada ya kutokea hali hiyo serikali imemuweka kwenye kizuizini cha nyumbani mwanamfalme huyo Hamzah huku maofisa kadhaa wa ngazi za juu nao wakitiwa nguvuni.

Hata hivyo, mwana mfalme Hamzah al-Hussein amesema atakaidi amri ya jeshi la nchi hiyo linalomtaka akaye kimya akiwa kwenye kizuizi cha nyumbani.

Hata hivyo sauti ya mwana Mfalme huyo iliyotumwa mtandaoni inaelezea kwamba hatakubali kuzuiwa kutoka nje, kutuma ujumbe kwenye ukurasa wa Twitter na ama kuwasiliana na watu wengine.

Mwanamfalme huyo ni ndugu wa baba mmoja wa mfalme Abdullah wa Pili wa Jordan yupo kizuizini lakini serikali ya Jordan imezuwia jaribio la mapinduzi, ingawa haikumtaja Hamzah kuhusika na jaribio hilo.

Mama yake mwanamfalme Hamzah, Malkia Noor, ambaye ana asili ya Marekani, amethibitisha kuwa mwanawe yuko kwenye kizuizi cha nyumbani alichoekewa na serikali ya Jordan.

Malkia Noor amelaani mwanawe kuekwa kizuizini na kueleza kuwa kinachofanyika ni fitna ovu dhidi ya mwanawe.

“Naomba ukweli na haki visimame kwa waathirika wote wasiokuwa na hatia wa fitina hii ovu. Mungu awabariki na kuwahifadhi,” kupitia mtandao wa Twitter.

Hata hivyo, jeshi la Jordan lilikanusha kumshikilia mwana Mfalme Hamzah, badala yake likasema kilichofanyika hasa ni kumtaka mrithi huyo wa zamani wa kiti cha ufalme.

Jeshi hilo lilieleza kuwa limemtaka mwanamfamlme huyo kuacha baadhi ya shughuli ambazo zingeliweza kuyumbisha utulivu na usalama wa nchi, lakini gazeti la Washington Post liliripoti kwamba kulikuwa na jaribio la kumuangusha mfalme Abdullah wa Pili, ambaye ni ndugu wa baba mmoja wa mwana Mfalme Hamzah.

Picha za video zilizotumwa mtandaoni zinaonesha kiwango kikubwa cha polisi kwenye eneo la Dabouq lililo karibu na makasri ya kifalme Abdullah liliopo mjini Amman, huku Mwana mfalme Hamzah bin Hussein akisema amezingirwa kwenye nyumba yake.

Kupitia ukanda wa video ambao baadhi ya mashirika ya habari ya kimataifa yameupata kutoka kwa wakili wake imeonesha kuwa mwana mfalme huyo alisema marafiki zake kadhaa wamekamatwa, walinzi wake kuondoshwa na huduma za simu na intaneti amekatiwa.

Mwanamfalme Hamzah, alikuwa ndiye mrithi wa ufalme wa Jordan, kabla ya Mfalme Abdullah kuchukua nafasi hiyo, lakini inasemekana taraibu zilikiukwa zilizomfanya kuikosa nafasi hiyo ya utawala nchini humo.

Mwana Mfalme Hamzah, ambaye ni ndugu wa baba mmoja na Mfalme Abdullah wa Pili, alikanusha kuwa sehemu ya njama ama kundi lolote la kihalifu.

Naongeza kueleza kuwa ufalme huo wa Kishamiyyah umegeuka kisima cha ufisadi, upendeleo wa kidugu na uongozi mbaya na kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kuwakosoa maovu yanayofanywa na waliomamlakani.

Gazeti rasmi la serikali nchini Jordan la Al-Rai, lilichapisha Aprili 4 mwaka huu lilieleza kuwa kwamba suala la usalama na utulivu wa nchi hiyo ni mstari mwekundu ambao haupaswi kuvuukwa au hata kukaribiwa”, na kwamba taarifa rasmi ya serikali ingelitolewa baadaye.

Shirika rasmi la habari la Jordan, Petra, liliwataja wasaidizi wa zamani wa familia ya kifalme akiwemo aliyekuwa mkuu wa utawala baina ya mwaka 2007 na 2008, Bassem Awadallah, pamoja na Sherif Hassan bin Zaid kuwa miongoni mwa watu wanaoshikiliwa.

Shirika hilo lilinukuu chanzo kimoja cha usalama, shirika hilo lilisema kuwa wawili hao walikamatwa kwa kwa sababu za kiusalama.

Hamzah ana mahusiano mazuri rasmi na ndugu yake Abdullah na ni mashuhuri sana miongoni mwa makabila ya Jordan.

Mfalme Abdullah alimteuwa Hamzah kuwa mrithi wa kiti cha ufalme mwaka 1999 kwa kutekeleza usia wa baba yao, lakini mwaka 2004 akamvua wadhifa huo na kumpa mwanawe wa kwanza wa kiume, aitwaye Hussein.