KIUNGO wa Real Madrid, Marco Asensio akifunga goli dhidi ya Liverpool kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa uwanja wa Alfredo di Stefano. Liverpool ilitandikwa 3-1.(DAILY MAIL).

WACHEZAJI wa Liverpool wakipigwa na mshangao baada ya kukubali kichapo mbele ya Real Madrid.

BOSI wa Real Madrid, Zinedine Zidane, akimpongeza winga wake raia wa Brazil,Vinicius Junior baada ya kufunga magoli mawili dhidi ya Liverpool.

MLINDA mlango wa Manchester City, Ederson akiwania mpira na kiungo wa Borussia Dortmund,Marco Reus kwenye uwanja wa Etihad. ManCity ilishinda 2-1.

NYOTA wa Dortmund, Marco Reus na Erling Haaland wakishangiria baada ya kufunga goli dhidi ya ManCity.

MWAMUZI, Ovidiu Hategan, akiangalia ‘VAR’ kujiridhisha baada ya awali kuizawadia ManCity mkwaju wa penalti kabla ya kubadilisha uamuzi huo.
