NA ZAINAB ATUPAE

VIONGOZI wa timu ya Mlandege wametakiwa kuwa karibu na wachezaji wao,ili kuwapa moyo kupambana na kushinda mechi zilizobakia kuiokoa klabu hiyo isishuke daraja.

Wito huo ulitolewa na kocha mkuu wa timu hiyo Ali Khalid’Kisoda’alipokuwa akizungumza na gazeti hili.

Alisema kuna umuhimu mkubwa viongozi wa timu hiyo kukutana na kukaa pamoja na wachezaji kuzungumzia matatizo yao na kuyafanyia kazi.

Akizungumzia kufanya vibaya kwa timu hiyo,alisema wachezaji wengi wa Zanzibar hawana malengo ,jambo ambalo linarejesha nyuma timu zao.

Mlandege hadi sasa ina pointi 17 ikishika nafasi ya pili kutoka mwisho ambapo wapinzani wao KMKM wanaongoza ligi ikiwa na pointi 32.