NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Polisi Tanzania, kinatarajia kushuka dimbani kuvaana na Biashara United leo Aprili 9 mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara.

Kikosi hicho kimeondoka juzi alfajiri kuelekea Mkoani Musoma kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano utakaopigwa katika dimba la Karume mkoani huko.

Kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Mkoani Kilimanjoro, Polisi wakiwa wenyeji wa mchezo huo ulimalizika kwa Biashara kupata ushindi wa bao 1-0.

Akizungumza na Zanzibar Leo, Ofisa Habari wa klabu hiyo Hassan Kayoza alisema timu imesafiri na jumla ya wachezaji 20.

Alisema baadhi ya wachezaji wamesimamishwa kucheza kutokana na utovu wa nidhamu mpaka uongozi utakapo kutana kuzungumza ndio itajulikana hatma yao.

“ Tumesafiri jana tupo mkoani Musoma tumekuja kucheza na Biashara, kikosi kilicho safari niwachezaji 20 wengine wamesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu,” alisema