NA ALLY HASSANI, DOMECO

JESHI la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, limefanikiwa kudhibiti ajali za barabarani katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ndani ya mwaka huu.

Akizungumza na Zanzibar Leo kwa njia ya simu, Inspekta Jabir Hassan, kwa niaba ya RTO wa Mkoa huo, alisema, ilivyozoeleka ndani ya mwezi wa Ramadhani zilizopita katika kipindi kama hichi huripotiwa ajali nyingi hasa wakati wa jioni watu wanapo kwenda kupata futari.

Inspekta Jabir alisema, hadi kufikia mwezi nane ndani ya Ramadhan ya mwaka huu, hakuna ajali yoyote iliyoripotiwa ndani ya Mkoa wa Mjini Magharib.

Alisema hali hio nikutokana na kupunguwa kwa misongamano barabarani iliyokuwa ikifanyika ndani ya Ramadhani ya miaka iliopita, ikilinganishwa na kipindi hichi kiasi kwamba limekuwa muarubaini wa kusaidia kupunguza ajali zinazo jitokeza.

“Kwenye kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani tumejipanga ipasavyo kudhibiti ajali zisitokee haswa muda ule wajioni ambao watu wanaenda kufutari,” alisema.

Alisema Jeshi hilo limejipanga kudhibiti maeneo hatarishi katika Mkoaa huo kwa kuweka askari ili kuzikabili hali zote zitakazo jitokeza katika wakati huo kama za kihalifu au za ajali.

Aidhaa inspekta huyo aliwataka madereva wanao endesha vyombo vya moto barabarani kutii amri bila kushurutishwa na kufuata sheria za barabara zilizowekwa ili kuepuka ajali zinazojitokeza kizembe.

Nao Madereva wanao endesha vyombo vya moto walisema, sehemu kubwa y ajali zinazotokea ni uzembe unao sababishwa na madereva kwenda mwendo kasi ambapo ndio chanzo kikuu kinacho pelekea ajali hizo kutokea kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramdhani.

Abuubakar Khamisi Kibwana dereva wa magari, alisema ndani ya mji wa Mjini Magharibi barabara, zimewekwa vibango ambavyo vinaonyesha viwango anavyotakiwa dereva kuendesha chombo chake, ila kuna baadhi ya madereva huendesha kinyume na kiwango kilicho wekwa.

Dereva huyo, aliwataka madereva wenzake wazingatie sheria za barabarani pia wawe makini wakati wanaendesha vyombo vyao, ili kuepukana na ajali zinazoweza kuepukika haswa wakati wa jioni, ambao unaonekana ajali nyingi zinatokea katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Abdurahmani Abdallah Juma alisema anaiomba serekali kuweka vifaa vitakavyo weza kupima mwendo kasi wa madereva wazembe wasio fuata sheria na taratibu za barabarani.