NA SAIDA ISSA, DODOMA
KAMANDA wa Polisi Jijini Dodoma amewaonya wananchi wenye nia ovu ya kufanya utapeli kwenye mkutano wakati maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakiendelea.

Mkutano Mkuu wa CCM unatarajiwa kufanyika April 30, mwaka huu, jijini Dodoma ambapo wajumbe wa Chama pamoja na wegeni  kutoka mikoa mbalimbali wanatarajiwa kuwepo.

“Nitoe onyo wale wanaokuja kama matapeli ambao wanavaa magwanda ya CCM laikini siyo wajumbe kumbe ni matapeli, wengine watajifanya usalama wa Taifa ,hao wote tutakuwa tunawachunguza, lakini cha zaidi ni kuhakikisha wanaoingia ni nwajumbe halali na siyo wajumbe
feki,”alisema Kamanda Muroto.

 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda Gilles Murotto alisema, wale wote waliojipanga kuingia Dodoma kwa ajili ya kufanya utapeli hawatatoka salama.

“Tunaepoelekea kwenye mkutano Mkuu wa CCM Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma, linaendelea na operesheni mbalimbali ikiwemo kuhakikisha wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wataoingia watakaa salama kipindi chote
cha Mkutano huo” alisema Kamanda Muroto.

“Wapo watakaojifanya wanaCCM watavaa sare za chama hicho lakini ni kwa nia ya kufanya utapeli ,wote hawa wataingia Dodoma lakini hawatatoka salama kwa sababu tumejipanga kikamilifu kuhakikisha Dodoma
inakuwa salama kipindi chote,”alisisitiza Kamanda.

Pia alisema, katika operesheni zake za kawaida jeshi hilo
limefanikiwa kukamata madereva bodaboda wanaohisiwa kujiingiza kwenye uhalifu pamoja na pikipiki 16.

Aidha, amekamatwa mtuhumiwa mmoja fundi pikipiki ambaye amekuwa akipelekewa pikipiki na kuzibadilisha vifaa kwa lengo la kuondoa muonekano wake wa mwanzo.

“Huyu tumemkamata na kazi yake ni kubadilisha vifaa vya pikipiki ili kuiondoa muonekano wa mwanzo utakaomfanya mwenye pikipiki kushindwa kuitambua, tunamshikilia ili atuambie pikipiki alizozifungua vifaa amezipata wapi.” alisisitiza Kamanda Muroto