MOSCOW, URUSI

RAIS wa Urusi Vladimir Putin, jana alifanya mazungumzo kwa simu na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, akiahidi kutoa msaada wa dharura wa matibabu kwa India iliyokumbwa na janga la Corona.

Putin alimwambia Modi kuwa  wakati nchi ya Asia Kusini inakumbwa sana na ongezeko kubwa la maambukizo ya COVID-19 ni lazima njia za haraka za misaada kupelekwa. Taarifa ya Kremlin ilisema kwa waandishi wa habari.

Alimwambia Modi kwamba Wizara ya Dharura ya Urusi itafanya safari za ndege wiki hii kupeleka zaidi ya tani 22 za vifaa kwa India, pamoja na wazalishaji 20 wa oksijeni, vifaa vya kupumulia 75, wachunguzi 150 wa matibabu na katuni 200,000 za dawa.

Kwa upande wake Modi alishukuru uamuzi wa Urusi na kwamba alisema anakaribisha misaada mbalimbali ya kiutu ya kukabiliana na janga la corona nchini mwake.