OUAGADOUGOU, BURKINAFASSO
WATU wanne wakiwemo raia wa kigeni watatu hawajulikani walipo baada ya kundi la wenye kujihami kwa silaha kukabiliana na kikosi cha doria cha kupambana na ujangili huko mashariki mwa Burkina Faso.
Mkasa huo umetokea wakati watu hao wakiwa njiani kuelekea katika eneo la hifadhi ya msitu wa Pama.
Na chanzo kimoja kimewataja waliopotea kuwa afisa jeshi la Burikina Faso, raia wawili wa Uhispania na mwingine kutoka Ireland.
hadi sasa hakujwa na taarifa yoyote kutoka mamlaka nchini humo au hata wizara ya mambo ya nje ya Uhispania.
Hata hivyo, inaaminika kwamba makundi ya wapiganaji wenye itikadi kali yanawashikilia mateka raia wa kigeni katika eneo zima la ukanda wa Sahel, kuanzia Burkina Faso, Mali hadi Niger.