NA MADINA ISSA
MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadidi Rashid, amefanya uteuzi wa Masheha wa Wilaya ya Kusini na Wilaya ya kati.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Salum Kassim Ali, imesema uteuzi huo umefanyika chini ya kifungu nambari 8 (1) cha sheria ya Tawala za Mikoa Namba 8 ya mwaka 2014.
Masheha walioteuliwa Wilaya ya Kati, Ali Juma Haji kuwa sheha wa shehia ya Mitakawani, Khamis Yagunga Shaaban sheha wa Pagali, Jafar Kheir Khatib shehia ya Pongwe, shehia ya Kaebona ni Shaka Haji Khamis, na shehia ya Chwaka Ali Hassan Mjombo.
Kwa upande wa Wilaya ya Kusini, Ajali Haru Abdallah kuwa sheha wa Michanvi, Mohammed Issa Nahoda kuwa sheha wa Mtende, Zaituni Bahorera Rajab Kajengwa na Mwachum Shaka Ali kuwa sheha wa Shehia ya Kizimkazi Mkunguni.
Hata hivyo, taarifa hiyo imesema kuwa uteuzi huo umeanza Machi 30, mwaka huu.