Na Mwandishi Wetu, zanzibar
RAIS Samia Suluhu Hassan, ametajwa kutokana na ukomavu wake katika medani za kisiasa, uongozi na utawala atabaki kuwa nguzo imara kwa hatma na mustakabali utakaodumisha Muungamo wa Tanganyika na Zanzibar .
Pia Rais huyo wa awamu ya sita amesifiwa akitajwa ni mwenye mahusiano thabit na mashrika ya kimataifa, mataifa washirika kwa maendeleo aliyejaaliwa ushawishi na mvuto kwa wawekezaji .
Hayo yamebainishwa jana na Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Kaskazini Unguja, Saada Mansour Hussein, aliyesema hana hofu wala kitete cha kuyumba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Samia, kwani anazielewa vyema siasa zake, kero na njia za kufikia utatuzi.
Saada alisema kiongozi huyo amepata uzoefu toka akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais Muungano na kabla ya hapo amekuwa Waziri wa Utalii na Uwekezaji SMZ kabla hajawa Naibu spika wa Bunge Maalum la Katiba mahali ambako alipoonyesha ukakamavu wa misuli yake ya ufahamu zaidi wa siasa na uongozi.
Alisema kudumu na kuwepo kwa muungano imara wenye usawa na heshima, ni uhakika na usalama kwa ustawi wa maisha ya watu na mali zao, kuendeleza udugu , kuimarika biashara na ,masoko , kuendelea kwa ushurikiano huku taifa likibaki moja bila kugawanyika.
“Tumempata mrithi sahihi wa kiti cha Urais mwenye uwezo, upeo na ufahamu. Ni kiongozi makini ,hodari na mchapakazi. Amepata uzoefu na kukomaa kisiasa na kiutawala.Rais samia atakuwa nguzo imara kwa mustakabli na hatma ya muungano wetu “Alisema Saada.
Aidha Mbunge huyo alisema kiongozi mwanamke aliyepata nafasi ya kuwa Rais awanu ya sita alimtaja ni mtulivu ,msikivu na mvumilivu kwani hupendelea kuendesha mambo kwa njia ya majadiliano kwa hoja mezani hadi kufikia tamati na muafaka kwani haamini kama jazba na pupa huleta suluhisho .
Kadhalika Mbunge huyo aliwataka wanawake wote nchini bila kujali vyama vyao sasa waweke pembeni tofauti zao za kisiasa na kuona huu ni wakati muhimu kwa wanawake wote kusimama pamoja na kuanza kuvuta kamba ya umoja na ushirikiano.
‘Wanawake wote duniani walipambana kupinga mifumo yote dume iliokandamiza haki za wanawake .Haitawezekana kila mwanamke ashike nafasi ya juu kwa wakati mmoja. Mwenzetu au kuwa wabunge .Mmoja anapofanikiwa ihesabike huo ni ushindI wa wanawake wote nchini “Alisisitiza saada
Vile vile alisema kwa miaka mingi duniani ilimuona mwanamke ni mtu wa mwisho anayestahili kukosa haki
Ilitosha ababaki nyumbani, akionekana ni nyenzo ya uzalishajimali katika kila familia akiwa kama mhudumu wa familia huiu akizalishwa bila kufuata uzazi wa mpango na uzazi salama.