COLOMBO, SRILANKA

WAZIRI mkuu wa Sri Lanka na wabunge jana waliadhimisha kumbukumbu ya pili ya mashambulio ya kigaidi ya Jumapili ya Pasaka kwa kukaa kimya kwa dakika mbili ili kuwakumbaka wahanga waliouawa katika milipuko ya kujitoa muhanga mnamo mwaka 2019.

Waziri Mkuu Mahinda Rajapaksa, alikaa kimya kwa heshima ya wale waliouawa katika makazi yake rasmi huko Colombo wakati wabunge ambao wote walikuwa wamevaa nguo nyeusi nao walikaa kimya katika uwanja wa bunge kabla ya vikao vya bunge vya siku hiyo.

Wakati huo huo, maelfu ya watu walikusanyika makanisani na wengine kwenda makaburini kwa ajili ya kuwakumbuka waliouawa katika mashambulizi hayo.

Zaidi ya watu 260 waliouawa katika milipuko hiyo na washambuliaji wa kujitoa muhanga mapema Aprili 21, 2019.

Matukio hayo yalifanyika chini ya usalama mkali wakati maelfu ya polisi na wanajeshi waliopelekwa katika kila kanisa kote nchini humo.

Mamlaka ya Sri Lanka inaendelea kuchunguza mashambulio ya kigaidi na inasema wamebaini wale waliosababisha shambulio hilo, ambao wamewekwa chini ya ulinzi.

Watalii kadhaa wa kigeni pia waliuawa katika mashambulio hayo