KAMPALA, UGANDA

TAARIFA kutoka nchini Uganda zinaeleza kuwa askofu wa jimbo la Kampala, Cyprian Kizito Lwanga akiwa kwenye za mwisho kabla ya kufariki alikuwa katika makaazi yake akitengeneza hotuba atakayoitoa kwa ajili ya pasaka.

Kwa mujibu wa taarifa askofu huyo alikuwa kwenye makaazi yake yaliyopo Rubaga akiandaa hotuba za sikukuu ya pasaka, kabla ya kufikwa na mauti ghafla Jumamosi iliyopita.

Vyanzo vya taarifa vilivyo karibu na askofu huyo vilieleza kuwa kwa muda wa siku kadhaa alikuwa akitekeleza ibada ya funga kabla ya kuingia kwa sikukuu ya pasaka.

Aidha taarifa zinaeleza kuwa askofu Cyprian Kizito Lwanga alikuwa na tatizo la muda mrefu la ugonjwa wa shindikizo la damu na ndio uliosababisha kifo chake kilichotokea ghafla.

“Tunaelewa kuwa ana tatizo la muda mrefu la ugonjwa wa presha lakini hakulalamika kuwa na maumivu ya aina yoyote”, alisema mmoja kati ya waumini walio karibu na askofu huyo. Habari ambao hazikutbitishwa na gazeti l