Gianluigi Donnarumma
KLABU ya Chelsea, Manchester United, Juventus na Real Madrid bado zinamtafuta mlinda mlango wa Italia, Gianluigi Donnarumma (22), ambaye amekataa ofa mbili za mkataba mpya AC Milan. (Gianluca di Marzio).
Lionel Messi
MANCHESTER City inafuatilia kwa karibu kuwasajili mshambuliaji wa Barcelona na Argentine, Lionel Messi (33), na mshambuliaji wa Borussia Dortmund, raia wa Norway, Erling Braut Haaland (20) katika uwanja wa Etihad. (Sun).
Paulo Dybala
KIUNGO wa Ufaransa, Paul Pogba huenda akaondoka Manchester United hata pengine msimu huu huku Juventus ikiwa makini kumsajili mchezaji huyo na pia nia ya kumuuza mshambuliaji wa Argentina, Paulo Dybala (27), katika makubaliano ya mabadilishano. (Tuttosport).
Harry Kane
KLABU ya Tottenham ina imani kubwa kwamba itaendelea kuwa na mshambuliaji wa England, Harry Kane (27), na haina mpango wa kumuuuza katika klabu nyengine ya Ligi Kuu ya England huku Manchester City Manchester United zikiendelea kumnyatia. (Manchester Evening News).
Son Heung-min
BAYERN Munich inamsaka mshambuliaji wa Tottenham, Son Heung-min (28), na ipo tayari kumsubiri mchezaji huyo wa Korea Kusini ambaye sasa hivi yuko Spurs hadi msimu wa mwaka 2023 na pia amepewa ofa ya makubaliano ya muda mrefu na klabu hiyo ya London. (Football Insider).
Georginio Wijnaldum
KLABU ya Barcelona inaonekana kuwa yenye uwezekano mkubwa wa kumsajili mlinzi, Georginio Wijnaldum (30), mkataba wake na Liverpool utakapomalizika msimu huu, lakini, klabu hiyo ya Catalanya inakabiliana na ushindani kutoka Chelsea, Juventus na Paris St-Germain. Klabu hiyo ya Merseyside bado haijakata tamaa ya kuendelea kusalia kuwa wa mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Uholanzi. (Marca).
Andros Townsend
WINGA wa Crystal Palace, Andros Townsend (29), amesema, klabu hiyo imemuarifu yeye pamoja na wachezaji wengine ambao hawana mkataba kwamba hatma zao hazitajadiliwa hadi mwisho wa msimu. (Talksport).
Sergio Aguero
MSHAMBULIAJI, Sergio Aguero (32), atakuwa bora zaidi kusajiliwa Juventus na huenda mchezo wake ukafikia kiwango cha mchezaji mwenzake aliyekuwa Manchester City na wa Argentina, Carlos Tevez huko Turin, amesema, mkongwe wa Juve, Franco Causio. (Gazzetta Dello).
Rodrigo
MSHAMBULIAJI wa Leeds United raia wa Hispania, Rodrigo (30), ametupilia mbali uvumi kuwa hana furaha Elland Road na kwamba anafuatilia kwa makini kurejea ‘La Liga’ baada tu ya msimu mmoja. (Leeds Live).
Carlos Tevez
MSHAMBULIAJI wa Boca Juniors, Carlos Tevez (37), ambaye ana miezi 12 kuamua ikiwa ataendeleza mkataba wake na mabingwa wa Argentina baada ya msimu huu, anahusishwa na kuhamia Marekani. (ESPN).
Christopher Schindler
KLABU ya Nuremberg ina panga kumsajili beki wa kati wa Huddersfield Town, Christopher Schindler (30), mkataba wake na miamba hiyo ya Ujerumani utakapokamilika msimu huu. (Bild).
Sean Dyche
KOCHA wa Burnley, Sean Dyche anaonekana kuwa mgombea ambaye anaongoza katika kinyanganyiro cha kumtafuta kocha mpya wa Crystal Palace ikiwa Roy Hodgson (73), hataongeza mkataba wake baada ya msimu huu. (90min).
Donny van de Beek
KLABU ya Manchester United iko tayari kutoa ofa kwa kiungo raia wa Uholanzi, Donny van de Beek (23) ya kumuuza Juventus kama sehemu ya makubaliano ya mabadilishano ya kumsajili mchezaji wa kimataifa raia wa Ufaransa, Adrien Rabiot (25). (Tuttosport).
Dael Fry
KLABU ya Burnley ina panga itakavyofanikisha uhamisho wa pauni milioni 10 kwa mlinzi wa Middlesbrough ambaye pia alikuwa katika timu ya England chini ya umri wa miaka 21, Dael Fry (23). (Mail).
Giorgio Chiellini
MLINZI wa Italia, Giorgio Chiellini, yuko tayari kusalia Juventus hata baada ya mkataba wake kukamilika msimu huu, amesema wakala wake, Davide Lippi, lakini, klabu hiyo ya Turin bado haijampa mkataba mpya. (Sky Italia).
Miguel Gutierrez
REAL Madrid imekataa ofa ya Tottenham baada ya klabu hiyo ya London kutaka kumsajili mlinzi wake raia wa Hispania, Miguel Gutierrez (19). (DefensaCentral).