Billy Gilmour
KIUNGO wa Scotland, Billy Gilmour (19), ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Thomas Tuchel cha Chelsea katika kipindi cha nusu msimu baada ya kocha wake mpya kufurahishwa na mchezo wake wakati wa mazoezi. (London Evening Standard).

Duje Caleta-Car
LIVERPOOL ilikuwa na euro milioni 23 kama dau lao wakati inamwania beki wa kati wa Croatia, Duje Caleta-Car (24), kiwango kilichokataliwa na Marseille. (RMC Sport).

Dayot Upamecano
MTENDAJI Mkuu wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge, amesema, Liverpool na Chelsea ndiyo timu mbili za Ligi Kuu ya England ambazo zinashindana naye katika kumsajili mlinzi wa RB Leipzig raia wa Ufaransa, Dayot Upamecano (22). (Mirror).

Marcelo
LIVERPOOL imekosa kidogo tu fursa ya kumsajili beki wa kati wa Lyon, Marcelo, baada ya klabu hiyo ya Ufaransa kukumbwa na matatizo ya kuwa na majeruhi kulikowafanya kuamua kutomruhusu raia huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 33, kuhamia kwengineko. (Sun).

Neco Williams
LIVERPOOL ilikataa hatua ya mwisho ya Southampton ya kutaka kumsajili mlinzi wa Wales, Neco Williams (19), kwa mkopo. (Sky Sports).

Diego Costa
MANCHESTER City haikuwa na nia ya kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Hispania, Diego Costa kwa uhamisho wa bure licha ya mchezaji huyo aliyekuwa Chelsea (32), kuhusishwa na tetesi za kutaka kuhamia klabu hiyo. (Mail).

Edin Dzeko
MANCHSTER United haikufikiria kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Roma na Bosnia-Herzegovina, Edin Dzeko (34), ambaye alikuwa mshambuliaji wa Manchester City, wakati wa uhamisho mnamo mwezi Januari licha ya mapendekezo ya vyombo vya habari vya Italia. (Express).

Zinedine Zidane
KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane ni lazima ashinde Ligi ya Mabingwa ili awe na uhakika wa kuendelea kuwa kocha wa timu hiyo. (AS).

Brandon Williams
MANCHESTER United ilitupilia mbali nia ya Southampton, Newcastle na West Ham ya kutaka kumsajili, Brandon Williams kwa mkopo ili kuendelea kuwa na mlinzi huyo wa Uingereza hapo Old Trafford. (Sun).

Taylor Harwood-Bellis
KUENDELEA kujiamini kwa Manchester City katika safu ya kiungo kumeiwezesha kumruhusu mlinzi wa Uingereza, Taylor Harwood-Bellis (19), kujiunga na Blackburn kwa mkopo. (Manchester Evening News).

Matt Ritchie
KOCHA, Steve Bruce amemuambia Matt Ritchie ajitahidi zaidi baada ya siku ya mwisho ya uhamisho kwa winga huyo wa Scotland kuhamia Bournemouth kugonga mwamba. (Newcastle Chronicle).

Carney Chukwuemeka
KIUNGO wa Aston Villa mwenye umri wa miaka 17, Carney Chukwuemeka, anafuatiliwa na Manchester United na Liverpool. (Times).