NEYMAR
MSHAMBULIAJI wa Brazil Neymar, 29, ameingia makubaliano ya awali ya kuichezea Paris St-Germain mpaka mwaka 2026- na sasa klabu hiyo ya Ufaransa inafanya jitihada ya kufanya makubaliano kama hayo na mshambuliaji wa Kifaransa Kylian Mbappe,22. (Telefoot, via AS)

ERLING BRAUT HAALAND
MSHAMBULIAJI wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland anaweza kuigharimu klabu kiasi cha pauni milioni 34 zaidi kwa sababu wakala wake Mino Raiola na baba Alf-Inge wanahitaji pauni milioni 20 kwa kila kamisheni kama sehemu ya mkataba. (RAC1, via Marca)

LIONEL MESSI
LIONEL MESSI anasubiri kuona ombi la Laporta kwa ajili ya mustakabali wa Barcelona kabla ya kuamua kusalia kwenye klabu hiyo au kujiunga na PSG au Manchester City. (Mundo Deportivo-in Spanish)

ANGEL DI MARIA
ANGEL DI MARIA amesema angependa kucheza sambamba na Messi kwenye kikosi cha PSG ikiwa mshambuliaji huyo, 33 ataondoka Barcelona. (beIN Sports,via Goal)

BRENDAN RODGERS
KOCHA wa Leicester Brendan Rodgers ana matumaini ya kumsajili kiungo wa kati Mskoti Callum McGregor,27, kutoka klabu ya Celtic. (Sun)


DAVID MOYES
KOCHA wa West Ham David Moyes amesema klabu hiyo itasikiliza ofa kwa ajili ya wachezaji Declan Rice,22, na kiungo wa kati wa Jamhuri ya Czech Tomas Soucek,26, msimu huu wa joto. (Mirror)

OUSMANE DEMBELE
MANCHESTER UNITED na Juventus ni klabu vinavyoonesha nia zaidi ya kumnasa mshambuliaji wa Barcelona, Mfaransa Ousmane Dembele,23, lakini Liverpool na PSG nao wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyo. (Mundo Deportivo-in Spanish)

THOMAS TUCHEL
KOCHA wa Chelsea Thomas Tuchel amemrejesha beki wa kati Antonio Rudiger,23, kutoka mazoezini siku ya Jumapili baada ya kuzozana na mlinda mlango Kepa Arrizabalaga,26, baada ya kufungwa 5-2 na West Brom Jumamosi. (Telegraph-subscription required)

LUCAS VAZQUEZ
WINGA wa Uhispania Lucas Vazquez,29, ambaye mkataba wake na Real Madrid unakwisha mwishoni mwa msimu, atapatiwa mikataba na Manchester United, Chelsea,AC Milan na Bayern Munich. (ABC-in Spanish)

ALVARO MORATA
JUVENTUS hawana uwezekano wa kulipa pauni milioni 8.5 zaidi kwa Atletico Madrid kwa ajili ya kuongeza mkataba wa mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata kwa mwaka mmoja mwingine kwasababu ya changamoto za kifedha. (AS)

YERRY MINA
BEKI wa kati wa Everton na Colombia Yerry Mina,26, anataka kuhamia ligi ya Serie A msimu huu wa joto, huku Inter Milan na Fiorentina nao wakimtolea macho mchezaji huyo. (Sun)

OLE GUNNAR SOLSKJAER
KOCHA wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 32, hatajiunga nao baada ya mkataba wake na mahasimu wao Manchester City kumalizika mwishoni mwa msimu. (Goal)