Juan Foyth

KLABU ya Villarreal wana matumaini ya kumsajili mlinzi wa Tottenham, Juan Foyth (23), msimu huu kwa mkataba wa kudumu kwa kiasi cha chini ya ada ya pauni milioni 13.Kwa sasa mchezaji huyo anacheza kwa mkopo katika klabu hiyo.(Football Insider)

Kelechi Iheanacho
MSHAMBULIAJI wa Leicester City, Kelechi Iheanacho anatarajiwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.(Daily Mail).

Arkadiusz Milik
MSHAMBULIAJI,Arkadiusz Milik huenda akaishia Atletico Madrid au Juventus msimu huu wa joto.(Mundo Deportivo).

Milan Skriniar
KLABU ya Tottenham inakaribia kufikia makubaliano ya kumsaini, Milan Skriniar.
Miamba hiyo ya Ligi Kuu ya England inafanya mazungumzo na beki huyo wa Inter na wanaonekana kufikia makubaliano.(Football Insider).

Moise Kean
JUVENTUS inatarajia kumrudisha, Moise Kean, kwenye klabu hiyo kutoka Everton.
Kean aliuzwa Everton mnamo 2019, lakini, alijitahidi katika msimu wake wa kwanza na ‘ Toffees’ na alipelekwa kwa mkopo PSG msimu huu. (Tuttosport).

Kevin Cabral
KLABU ya LA Galaxy inajiandaa kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21, Kevin Cabral.( La Voix du Nord).

Jose Mourinho
JOSE Mourinho amesema anatarajia dirisha la ‘ajabu’ la uhamisho wakati akielezea mipango yake ya msimu wa joto.(Goal).

Ismaila ‘Ish’ Jome
KLABU ya Portland Timbers imemsaini beki Ismaila ‘Ish’ Jome na kiungo, Jorge Gonzalez.(AFP).

Vicente Sanchez
MKONGWE wa MLS, Vicente Sanchez amesainiwa na Rio Grande Valley FC.
Sanchez, ambaye mwanzoni alikuja MLS mnamo 2013, atatoka kwenye kustaafu kucheza wakati pia akihudumu kama mshiriki wa benchi la ufundi.(AFP).

Thomas Tuchel
THOMAS Tuchel, amesema, hana wasiwasi juu ya dirisha la uhamisho kwani anafurahi zaidi na kikosi chake cha sasa cha Chelsea.(Goal).

Nick Marsman
KLABU ya Inter Miami inataka kumsajili kipa wa Feyenoord, Nick Marsman.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 amemaliza mkataba msimu huu wa joto na anaangalia uhamisho wa MLS.(Votebel International).

Pep Guardiola
KOCHA, Pep Guardiola amesema Manchester City wanaweza kuamua kutumia zaidi ya pauni milioni 100 kwa ajili ya mchezaji mmoja siku za usoni, lakini ameendela kuwa na kigugumizi juu ya tetesi kuhusu klabu yake kuhusishwa na Haaland. (Sky Sports).

Zinedine Zidane
KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amevunja ukimya ukimya kuhusu tetesi za uhamisho zinazomuhusisha mshambuliaji wa Misri na Liverpool, Mohamed Salah (28), kuhamia Bernabeu. (Liverpool Echo).