MOHAMED SALAH

MABINGWA wa Ufaransa klabu ya Paris St-Germain wamefanya mawasiliano na wawakilishi wa mshambualiaji nyota wa Liverpool Mohamed Salah, 28, ili kumsajili mchezaji huyo tegemezi pia wa timu ya taifa ya Misri. (Telefoot on Twitter – in French)

MAURICIO POCHETTINO
KOCHA wa PSG Mauricio Pochettino pia amewasiliana na mshambuliaji nyota wa Tottenham na timu ya taifa ya England Harry Kane, 27, kuhusu uwezekano wa nyota huyo kuhamia Ufaransa. (Telefoot on Twitter – in French)

JURGEN KLOPP
MIAMBA ya soka nchini Ujerumani klabu ya Bayern Munich itajaribu kumsajili kocha wa Liverpool Jurgen Klopp mwishoni mwa msimu endapo kocha wao Hansi Flick ataenda kuitumikia timu ya Taifa ya Ujerumani. (90mins)

HERBERT HAINER
RAIS wa Bayern Herbert Hainer, anaamini Hansi Flick ataendelea kusalia katika klabu hiyo inayokipiga katika uga wa Allianz Arena. (Sky Sport Germany, via Goal)

JOSE MOURINHO
KOCHA wa Tottenham Hotspur Jose Mourinho anapanga kumsajili kiungo wa Ubelgiji Marouane Fellaini, 33, ambaye pia alikuwa chini yake katika klabu ya Manchester United. Fellaini kwa sasa yupo na klabu ya Shandong Luneng ya Uchina toka Februari 2019 alipoihama United.

BOUBAKARY SOUMARE
KLABU ya Leicester City ipo mbele ya Manchester United na katika mbio za kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Lille Boubakary Soumare, 22. (Star)

PAU TORRES
MANCHESTER UNITED wanamtaka ‘kwa udi na uvumba’ beki wa klabu ya Villarreal na Uhispania Pau Torres, 24, ambaye pia anawaniwa na vigogo wengine wa soka barani Ulaya klabu za Bayern Munich na Real Madrid. (AS, via Team Talk)

PAULO DYBALA
MAZUNGUMZO baina ya klabu ya Juventus na mshambuliaji wake Paulo Dybala 27 – ambaye anahusishwa na mipango ya kutaka kuhamia Manchester United – bado hayajakamilika kutokana na hali ya kifedha ya klabu hiyo ya Turino, ameeleza mkurugenzi wa ufundi wa wa klabu hiyo Fabio Paratici. (Sky Italia, via Goal)

EDINSON CAVANI
DAU la pauni milioni mbili kwenye mkataba wa mshambuliaji Edinson Cavani linaweza kuwa shubiri katika mipango ya mchezji huyo kuihama Manchester United mwishoni mwa msimu. Cavani, 34, amekuwa akihusishwa na mipango ya kuhamia klabu ya Boca Juniors. (Mirror)