JOSE MOURINHO
KUNA uwezekano mkubwa wa meneja wa Tottenham Jose Mourinho hatakuwepo kwenye klabu msimu ujao, Spurs ikijitahidi kupata nafasi ya ligi ya mabingwa kwa 2021-22. (Football London)
PAUL POGBA
KIUNGO wa kati wa Ufaransa Paul Pogba anataka pauni 500,000 kwa wiki kusaini mkataba mpya na Manchester United, wakati Real Madrid, Paris St-Germain na Juventus pia wameambiwa juu ya mahitaji ya mshahara wa mchezaji huyo wa miaka 28 ikiwa wanataka kumsajili. (Star on Sunday)
RAPHAEL VARANE
CHELSEA itachuana na Manchester United katika usajili wa mlinzi wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane, 27.(Bild journalist Christian Falk on Twitter)
RAHEEM STERLING
MSHAMBULIAJI wa Manchester City Raheem Sterling, 26, anavutia tena na Real Madrid, na mchezaji huyo wa kimataifa wa England alikuwa akihangaikia kupata namba kikosi cha kwanza katika wiki za hivi karibuni.
(Star on Sunday)
ADAMA TRAORE
WOLVES inataka kumtema winga wa Hispania, Adama Traore kusaidia kukusanya pesa za usajili mpya na pauni milioni 30 zinaweza kutosha kwa klabu kumsajili mchezaji huyo wa miaka 25.(Football Insider)
EMERSON
TOTTENHAM inaendelea kumfuatilia beki wa kulia wa miaka 22 wa Brazil Emerson, ambaye yuko mkopo Real Betis kutoka Barcelona.(Mundo Deportivo – in Spanish)
GEORGINIO WIJNALDUM
KIUNGO wa Liverpool, Georginio Wijnaldum, 30, amepanga kujiunga na Barcelona msimu huu wa joto kwa sababu anataka kucheza pamoja na Lionel Messi na mwenzake wa Uholanzi Memphis Depay.(Sunday Mirror)
TAMMY ABRAHAM
MSHAMBULIAJI wa England Tammy Abraham huko Chelsea yuko mashakani baada ya meneja Thomas Tuchel kumwacha mchezaji huyo wa miaka 23 nje ya kikosi cha ushindi wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester City.(Mail on Sunday)
FIKAYO TOMORI
AC MILAN imeweka wazi kwa Chelsea wana mpango wa kuchukua mlinzi wa England Fikayo Tomori mwenye umri wa miaka 23 kwa mkataba wa kudumu.
(Football Insider)
RUBEN LOFTUS-CHEEK
ASTON VILLA na Crystal Palace wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea na England 25, Ruben Loftus-Cheek, ambaye yuko kwa mkopo Fulham.
(Teamtalk)
NICOLAS TAGLIAFICO
LEEDS UNITED ina mpango wa kumhamisha beki wa kushoto wa Argentina mwenye umri wa miaka 28 Nicolas Tagliafico, ambaye mkataba wake na Ajax unaendelea hadi 2023. (Sunday Mirror)
ADAM HLOZEK
WEST HAM wanazidisha harakati zao za kumsajili mshambuliaji wa Sparta Prague Adam Hlozek, na mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech mwenye umri wa miaka 18 pia anavutiwa na klabu nyingine. (90 Min)
ALASSANE PLEA
MSHAMBULIAJI wa Ufaransa Alassane Plea yuko tayari kuondoka Borussia Monchengladbach, huku Arsenal, Leicester na West Ham wakiwa wameonyesha nia ya mchezaji huyo wa miaka 28. (Mail on Sunday)
PAPE SARR
MANCHESTER UNITED inaongoza harakati za kumsajili kiungo wa kati wa Metz na Senegal Pape Sarr, lakini klabu nyingine vinavutiwa na mchezaji huyo. (Sun on Sunday)