Max Aarons
KLABU ya West Ham wameungana na Barcelona, Bayern Munich na Tottenham katika kinyang’anyiro cha kumsaka beki wa Norwich City na England chini ya umri wa miaka 21, Max Aarons, huku klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England ikisemekana kuitisha angalau paundi milioni 30. (Independent).

Jadon Sancho
MATUMAINI ya Manchester United kumsajili mshambuliaji wa England, Jadon Sancho (21), kutoka Borussia Dortmund huenda yamepata nguvu mpya kutokana na taarifa kwamba naibu mwenyekiti, Ed Woodward anatarajiwa kuondoka klabu hiyo. (Star).

Ousmane Dembele
KLABU ya Juventus wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona, Ousmane Dembele (23), mkataba wake utakapoisha 2022.(Daily Mail).

Jesse Lingard
KLABU za Paris St-Germain, Real Madrid na Inter Milan zinamfuatilia winga Jesse Lingard tabla ya dirisha la usajiri halijafunguliwa mwishoni mwa msimu. Lingard, 28, anang’ara kwa sasa ambapo anachezea klabu ya West Ham kwa mkopo akitokea Manchester United. (ESPN).

Orkun Kokcu
KLABU ya Tottenham wamepanga kwenda uso kwa uso na Arsenal katika mbio za kumsajili, Orkun Kokcu kutoka Feyenoord.(Daily Mail).

Carlos Mendes
WINGA wa Morecambe, Carlos Mendes Gomes ameibuka kama mlengwa wa Ranger.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye alitumia muda na Atletico Madrid akiwa kijana, ametazamwa mara kadhaa na mabingwa wa Ligi Kuu kutoka Ibrox.(Sun).

Kalidou Koulibaly
KLABU ya Everton ni miongoni mwa vigogo vya Ligi Kuu ya England vinavyoangalia uhamisho kwa ajili ya Kalidou Koulibaly, lakini, Carlo Ancelotti amesema, beki huyo sio sehemu ya mipango yake majira ya kiangazi.(Goal).

Jerome Boateng
BEKI, Jerome Boateng sio mlengwa wa Barcelona.
Beki huyo aliyeshinda Kombe la Dunia anatarajiwa kuondoka Bayern Munich kama mchezaji huru msimu huu wa joto, lakini, Camp Nou hawana nia ya kumnasa kwani wanapendelea dili kwa David Alaba.(Mundo Deportivo).

Raphinha
KLABU ya Leeds bado hawajaona njia zozote zilizofanywa kwa ajili ya Raphinha.
Winga huyo wa Brazil ameona azma kutoka kwa Liverpool na Manchester United zikipingwa baada ya kutupiwa jicho wakati wa kampeni yake ya kwanza huko England.(The Athletic).

Edinson Cavani
MSHAMBULIAJI, Edinson Cavani, ameripotiwa kukaribia dili la uhamisho Boca Juniors, lakini, klabu hiyo haitatangaza hadi mwishoni mwa msimu.(Todo Fichajes).

Antonio Conte
KLABU ya Atletico Madrid inaweza kufikiria uhamisho kwa bosi wa Inter, Antonio Conte kumrithi Diego Simeone ikiwa mwisho atashawishiwa na klabu hiyo ya ‘Serie A’ kuchukua nafasi.(La Razon).

Odsonne Edouard
MSHAMBULIAJI, Odsonne Edouard anaweza kujiandaa na uhamisho wa makubaliano kutoka Celtic msimu huu wa joto wakati anaingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake.(Football Insider)

Mateo Mussachio
MATEO Mussachio anaweza kurudi ‘La Liga’ kufuatia kukaa ngumu huko ‘Serie A’, huku Real Betis ikitarajiwa kuwa makazi yake.(Todo Fichajes).

Moise Kean
KLABU ya Juventus inaweza kufanya uhamisho wa kumtwaa Moise Kean kufuatia kiwango anachokionesha akiwa kwa mkopo Paris Saint-Germain.
Miamba hiyo ya ‘Bianconeri’ inajiandaa kupoteza taji la ‘Serie A’ kwa mara ya kwanza katika muaongo mmoja na wanaangalia kujipanga upya.(Tuttosport).

Goncalo Guedes
KLABU ya Wolves inakusudia kuimarisha harakati zao kwa mshambuliaji wa Valencia, Goncalo Guedes, na wanaweza kumtumia Patrick Cutrone kwa kubadilishana.(Football Insider)