Abdallah Sima
MANCHESTER United wanamuwinda mshambuliaji wa klabu ya Slavia Prague, Msenegali Abdallah Sima (21). (Manchester Evening News).

Cristiano Ronaldo
KLABU ya Paris St-Germain wapo mbele ya Manchester United katika harakati za kumsajili mshambuliaji nyota wa Ureno na Juventus, Cristiano Ronaldo (36). (Tuttosport).

Julian Nagelsmann
KLABU ya RB Leipzig wanataka dau litakalovunja rekodi la usajili wa makocha la euro milioni 25 kutoka Bayern Munich ili kumuachia kocha wao, Julian Nagelsmann (Sky Sports).

Eric ten Hag
KLABU ya Tottenham sasa itaaelekeza nguvu kumsajili kocha wa Ajax, Eric ten Hag wakati huu ambapo Bayern inaonekana ipo mbioni kumsajili Nagelsmann. (Telegraph).

Gianluigi Donnarumma
MLINDA mlango wa Italia, Gianluigi Donnarumma (22), atasalia AC Milan licha ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu na kutakiwa na klabu za Manchester United na Chelsea. (TalkSport).

Raphael Varane
REAL Madrid hawatakaza msuli kumbakisha klabuni hapo beki wa Ufaransa, Raphael Varane (28), ambaye amekuwa akiwaniwa na Manchester United na Chelsea. (AS).

Xherdan Shaqiri
KIUNGO wa Uswisi, Xherdan Shaqiri (29), anataka kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu ili kupata sehemu atakayocheza zaidi. (Football Insider).

Emile Smith Rowe
ARSENAL wameanzisha mazungumzo na kiungo wao kinda, Emile Smith Rowe (20), ili kumpatia mkataba mpya. (The Athletic).

Andrew Moran
KLABU za Chelsea na Manchester United wanamuwinda kiungo kinda wa Brighton, Andrew Moran (17). (Team Talk).

Eric Garcia
Barcelona wanaimani kuwa Eric Garcia (20), atajiunga na klabu hiyo mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wa beki huyo na Manchester City unaelekea kufikia tamati. (Mundo Deportivo).

Maurizio Sarri
AS Roma imemchagua kocha wa zamani wa Chelsea na Juventus, Maurizio Sarri kuwa meneja wao mara baada ya msimu huu kukamilika. (Corriere dello Sport).