KARACHI, PAKISTAN

WAZIRI wa Mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov, amewasili nchini Pakistan kwa ziara ya siku mbili.

Waziri wa Mambo ya nje wa Pakistan, Shah Mahmood Qureshi, mwenyeji wake Lavrov wakati alipowasili.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Pakistan, ilisema kuwa ziara hiyo ya Lavrov inakusudia kuimarisha uhusiano baina ya nchi mbili hizo na masuala tofauti ya kiuchumi na kimaendeleo kwa nchi mbili hizo.

“Tunakusudia kuimarisha masuala ya kimkakati baina ya pande zote mbili na kwamba tutaimaisha miundombinu rafiki kuhakikisha tunafanikiwa”, alisema waziri wa mambo ya nje wa Pakistan Shah Mahmood.

Nae waziri wa mambo ya nje wa Urusi Lavrov, alisema nchi yake itaimarisha mahusiano yaliyopo ili kuhakikisha kuwa maendeleo ya nchi mbili hizo yanapatikana.

Mapema Qureshi alisema katika ujumbe maalum wa video kabla ya kuwasili kwa Lavrov kwamba uhusiano kati ya Pakistan na Urusi unaelekea mwelekeo mpya na matarajio ya biashara iliyoimarishwa na fursa za uwekezaji.