N’DJAMENA, CHAD

VIONGOZI mbalimbali wa kigeni wameshiriki katika mazishi ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Idriss Deby yaliyofanyika hapo jana.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, rais wa Guinea Alpha Conde na wakuu kadhaa wa nchi za kiafrika waliwasili mjini N’Djamena licha ya waasi kuwaonya viongozi wa kigeni kutohudhuria mazishi ya Debby yauyofanyika jana Ijumaa kwasababu za kiusalama.

Baada ya kutolewa kwa heshima za kijeshi na hotuba mbali mbali, sala zilifanyika katika msikiti wa Grand Mosque uliopo N’Djamena.

Baadaye , mwili wa Déby’s ulisafirishwa kwa ndege hadi Amdjarass, kijiji kidogo kilichopo karibu na mji anakotoka wa Berdoba, uliopo zaidi ya kilomita 1000 (maili 621) kutoka mji mkuu, karibu na mpaka wa Sudan.

Rais Déby alikuwa mtu muhimu katika mkakati wa usalama katika kanda ya Sahel.

Baraza la kijeshi linaloongozwa na mwanae, Jeneral Mahamat Idriss lilichukua madara baada ya kifo chake naanaungwa mkono kwa kiasi kidogo na jeshi lakini anauungwa mkono na mtawala wa Ufaransa.

 

Ufaransa inaiunga mkono serikali ya kijeshi katikati mwa kitisho cha waasi cha kufanya mashambulizi katika mji mkuu wa N’Djamena Baraza la kijeshi linaloongozwa na Jenerali Mahamat Idriss Deby mwenye umri wa miaka 37, lilichukua madaraka baada ya kifo cha baba yake ambaye ametawala kwa miaka 30 na alikuwa mshirika wa karibu wa mataifa ya magharibi.