JUBA, SUDAN KUSINI

WATU watano wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa wakati mtu mwenye bunduki aliposhambulia gari iliyokuwa ikisafiri kutoka nchini Sudan Kusini kueleka Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa zimeeleza kuwa shambulizi hilo limetokea katika barabara kuu itokayo Juba kuelekea Nimule, ambapo watu hao wakiwa katika gari ghafla walivamiwa na mtu mwenye bunduki na kuua watu hao kujeruhi.

Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini, amelishutumu kundi la waasi wa National Salvation Front (NAS) kuhusika na mauaji hayo.

Katika tukio jengine maofisa wa jeshi katika kuzuizi cha barabara ya Juba kuelekea Nimule alisema kuwa gari nyengine tatu zilivamiwa na watu wenye silaha majira ya saa 12 za asubuhi katika eneo la Kit 2.

Msemaji wa jeshi kwenye vizuizi hivyo kanali Santo Domic alisema gari ya kwanza ilifanikiwa kuwatoroka wavamizi pamoja na kwamba walishambuliwa lakini hakukutokea athari za mauaji wala majeruhi.

Alisema kuwa gari nyengine mbili zilinaswa na waasi hao na kufanikiwa kuwaua watu waliokwemo kwenye gari hizo na kuzichoma moto.

Kanali Santo alisema ni vigumu kwatambua watu waliokuwemo kwenye gari hizo kwani miili yao imeunga vibaya sana kiasi cha kutotambulika kabisa.

Jeshi la Sudan Kusini limeeleza kuwa makundi ya waasi yanahusika na mauaji hayo na kwamba wanaonesha kwamba bado wapo, na kueleza kuwa juhudi za kuwasaka zitachukuliwa.