YANGON, MYANMAR
SERIKALI ya Mynmar iliyo chini ya Jeshi imetoa agizo la kuachiliwa huru wafungwa wapatao 23,184 katika kile kilichoelezwa kuwa ni msamaha wa mwaka nchini humo.
Msemaji wa Idara ya Wafungwa nchini Myanmar alisema kuwa, kama kuna mwanaharakati yeyote aliyetiwa mbaroni kuanzia Februari 1 mwaka huu wakati jeshi lilipotwaa madaraka ya nchi basi atakuwa miongoni mwa walioachiliwa huru.
Hata hivyo baadhi ya ripoti zilisema kuwa, wengi wa walioachiliwa huru ni wale waliofungwa kabla ya matukio ya Februari 1.
Aidha taarifa zaidi zilisema kuwa, kuna raia wengi ambao walitiwa mbaroni katika maandamano ya kupinga hatua ya jeshi ya kutwaa madaraka ya nchi ambao hatima yao haijulikani, kwani hawamo katika orodha ya walioachiliwa huru.