RABAT, MOROCCO

JESHI la wanamaji la Morocco liliwaokoa mwishoni mwa wiki iliyopita wahamiaji 165 wa Uhispania katika Bahari ya Mediterania na Atlantiki, shirika la habari rasmi MAP liliripoti Jumatatu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la MAP, lilisema kuwa miongoni mwa wahamiaji waliookolewa walikuwa watu 103 wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, raia wa Morocco, 34, Bangladesh 27 na Burma mmoja.

“Walikuwa wakiwa katika hatari ya kuzama wakiwa katika boti kadhaa za zisizo madhubuti zilizokuwa zikisafiri katika  bahari ya Mediterania “, alisema.

Wahamiaji waliokolewa walipewa msaada wa haraka kutoka kwa vikosi vya uhamiaji kabla ya kurudishwa katika bandari za karibu za Moroco na kukabidhiwa kwa wahusika.

Morocco imekuwa ni lango kuu kwa wahamiaji wa Kiafrika na Asia wanaotafuta njia ya kuelekea Ulaya ili kupata maisha bora.

Aidha kutoka Morocco hadi Uhispania ni masafa mafupi kwa kutumia usafiri wa bahari ya Medditerania takriban kilomita 14 tu kupitia Mlango wa Gibraltar.