KINSHASA, DRC

WATU saba wameuawa na wengine 22 wamejeruhiwa katika maandamano yaliyofanyika wilayani Nyiragongo jimboni Kivu kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Tangu wiki iliyopita kulikuwa na maandamano mjini Beni, Butembo na Goma wakitaka kuondoshwa kwa vikosi vya UN kwa madai ya kushindwa kudhibiri makundi ya waasi yanaoendelea kuua watu.

”Mapigano yalianza Jumatatu baada ya watu wawili wa kabila la Kumu kukutwa wamekufa mauaji yanayodaiwa kufanywa na watu wa kabila la Nande” Waziri wa ulinzi jimboni humo Bosco Sebishyimbo.

Taarifa zinasema nyumba kadhaa zimeteketea kwa moto, katika mapigano kati ya kundi la waandamanaji na polisi Jumatatu katika mkoa wa Bukumu, eneo la Nyiragongo.

Katika miji ya Beni, Butembo na Goma kumekuwa na maandamano ya hivi karibuni dhidi ya mauaji na ukatili mwingine unaofanywa na vikundi vyenye silaha huko Beni na eneo hilo lina makazi ya walinda amani wengi wa UN (MONUSCO).

Picha za nyumba mpya na vijana walio na silaha za jadi na askari katikati ya mzozo zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha tukio hilo huko Buhene katika eneo la Majengo nje kidogo ya Goma.