KAMPALA, UGANDA
POLISI katika mji wa Mbale uliopo Uganda, unawashikilia watu wawili akiwemo mmoja raia wa kigeni kwa kukamatwa na dola milioni 500 za marekani ambazo ni feki.
Kwa mujibu wa polisi katika jiji hilo walieleza kuwa watu hao walikamatwa katika benki ya ABSA iliyopo katika mtaa wa Republic katika ambapo walikutwa na shehena kubwa ya fedha dola za marekani.
Polisi walisema watu hao walikuwa kwenye harakati za kutaka kuibadilisha fedha hizo na fedha za Uganda ili waziingize kwenye mzunguuko wa fedha.
Msemaji wa polisi katika mji wa Mbale, Rogers Taitika alisema mbali ya kukutwa na dola feki, pia wamekutwa na funguo zenye uwezo wa kufungua kufuli yoyote.
“Tunaendelea na uchunguzi, inaonekana huu ni mtandao na lazima tuwakamate wote wanaohusika na kuingiza fedha feki katika matumizi ya wananchi ya wananchi wa Uganda”, alisema Rogers Taitika.
Aliwataja waliohusika na kadha hiyo ni pamoja na Rashid Mudebo mwenye umri wa miaka 46 mkaazi wa kijiji cha Namanyonyi na Jackline Anzirini mwneye umri wa miaka 35 mkaazi wa Matayosi huko Busia nchini Kenya.
Aidha alisema wahalifu hao walikuwa wakitumia gari yenye nambari UBH 377F za usajili uchunguzi wao unaendelea na watafikishwa mahakamani taratibu zitakapokamilika.