MEXICO CITY, MEXICO

DARAJA liliporomoka hapo jana huko kusini mwa jiji la Mexico city lilisababisha vifo vya watu 13 na wengine 70 kujeruhiwa.

Taarifa kutoka eneo la tukio zilisema kuwa daraja hilo liliporomoka siku ya Jumatatu usiku.

Katibu wa serikali wa Jiji la Mexico, Alfonso Suarez del Real, aliwaambia waandishi wa habari kuwa vikosi vya dharura vilifika eneo la dharura, na kutoa huduma kwa wahanga wa tukio hilo.

Hadi hapo jana huduma za uokozi zilikuwa zikiendelea na kwamba walisema kuwa huenda idadi ya watu waliokufa ikaongzeka kwa kuwa bado watu wengine huenda wakafukiwa na vifusi huku baadhi ya majeruhi wakiwa katika hali mbaya.

Uchunguzi wa ajali hiyo bado unaendelea.