NA ZAINAB ATUPAE

MABAHARIA weusi Black Sailors wameondoka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Polisi katika mchezo wa kirafiki.

Mchezo huo uliotimua vumbi uwanja wa Mao Zedong ‘A’ majira ya saa 1:00 asubuhi ambao uliokuwa wa ushindani.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko  Black Saloirs ilikuwa ikiongoza kwa mabao mawili.

Mabao hayo yalifungwa na Abdulradhak Omar ‘Bale’ dakika ya 23 na bao la pili liliongezwa na Suleiman Ali Othman dakika ya 32.

Kurudi uwanjani kumalizia dakika zilizobakia timu hizo ziliingia na kasi kubwa ambapo dakika ya 56 Abdalla Mwalim wa Polisi alifunga bao la kufutia machozi.

Kuingia kwa bao hilo kuliwaongeza nguvu mabaharia weusi dakika ya 78 Yussuf Hassan Issa alipata nafasi ya kuongeza bao la tatu ambao yalidumu hadi mwisho wa mchezo.

Ligi kuu ya Zanzibar inatarajiwa kuanza Mei 22 baada ya kupisha mwezi mtufu wa Ramadhan na sikukuu.