NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara Almasi Kasongo,amesema kupeleka mbele baadhi ya michezo ya ligi kuu ni kutoa nafasi kwa baadhi ya timu kumaliza viporo vyao.

Hivi karibuni baadhi ya makocha wamekuwa wakilalamika timu kukaa mwezi mmoja pasina kucheza mechi bila sababu za msingi.

Akizungumza na Zanzibar Leo jana Kasongo alisema lengo kuu la kupanga ratiba mpya na kupeleka mbele,baadhi ya michezo ya timu ni kutaka timu zenye viporo kumaliza.

Alisema si jambo zuri kuona baadhi ya timu zinamaliza ligi na wengine bado, hivyo wameamua kufanya mabadiliko hayo ili timu zenye viporo ziweze kumaliza viporo na wanaocheza michezo ya Kombe la Shirikisho wataendelea na ratiba mpya.

“Ni kweli michezo mingi imesogezwa mbele, sio sahihi timu kuwa na viporo vingi, hawa wanacheza hawa wamemaliza sio sawa hivyo watamaliza kwa pamoja,” alisema