NA JUMA RAMADHAN, OUT-PEMBA

HATIMAYE volcano iiliyokuwa ikiripuka katika mlima Nyiragongo imepoa, hata hivyo matope ya mato yamesababisha athari kubwa.

Mlima huo ni miongoni mwa milima yenye volcano iliyo hai, hata hivyo kumekuwa na hofu kwamba umekuwa hauchunguzwi ipasavyo, hali iliyosababisha wananchi kushitukiza wakitakiwa waondoke eneo hilo kupisha mripuko wa volcano.

Kazi ya uchunguzi wa kijiolojia wa mlima huo, ipo chini ya taasisi ya uangalizi wa volkano ya Goma, ambayo ilikatiwa ufadhili wa kifedha na Benki ya Dunia kutokana na kukithiri kwa madai ya ufisadi katika taasisi hiyo.

Dalili za kulipuka kwa volkano hiyo katika miaka ya hivi karibuni zilikuwa zipo wazi kwa muda mrefu.

Mwaka jana Mkurugenzi wa uangalizi wa mlima huo, Katcho Karume aliiambia BBC kuwa, ziwa la lava ya volcano limekuwa likijaa haraka na hivyo kuongeza uwezekano wa kulipuka, katika miaka michache ijayo.

Ingawa alionya kuwa tetemeko la ardhi linaweza kusababisha maafa mapema katika eneo hilo. Katika ripoti ya Mei 10 mwaka huu, waangalizi walionya kwamba mitetemo ya chini ya ardhi, katika mlima Nyiragongo ilikuwa imeongezeka.

Sasa kwa nini tahadhari haikutolewa kwa jamii mpaka mlipuko ukatokea na wananchi ikawalazimu kujihami kwa kukimbia makaazi yao bila maelekezo ya kitaalamu?

Shirika la Utangazaji la Uengereza la Kiswahili la ‘BBC’ limezungumza na Kasereka Mahinda Celestine, ambae ni ofisa Mwandamzi wa taasisi ya volkano ya Goma.

Ambapo pamoja na hayo, yeye alikiri kuwa ukata wa kifedha umeathiri kazi zao, kwa kiwango kikubwa, japo anakiri bado tahadhari ingeweza kutoka mapema.

Inasemakana kulikuwa na dalili za kurupuka lakini kuna kipindi tumepita bila ya matumizi (ya pesa), takribani kwa miezi sita mambo hayatembei vizuri kwa kazi juu ya ukosefu wa pesa.

Baada ya kupata msaada na kuanza kazi kuona hiyo dalili na kuandaa ilani kumbe, (hatari) ilikuwa mbele zaidi.

Baada ya kutoa tahadhari viongozi wanatakiwa kutoa mpango kwa wakaazi lakini inaonekana kuwa hatukusisitiza (hali ya hatari) katika ripoti yetu ya kila baada ya wiki mbili kwa viongozi,” amekiri bwana Mahinda.

Mlima huo wa volkano uliopo kilomita 10 (maili sita) kutoka Goma, ulilipuka mara ya mwisho mwaka 2002 na kusababisha vifo vya watu 250 huku watu wengine 120,000 wakiachwa bila makazi.

Mlipuko wa volkano uliosababisha vifo zaidi ulitokea mwaka 1977, ambapo watu 600 waliuawa.

Profesa Mike Burton, mtaalamu wa masuala ya volkano katika Chuo Kikuu cha Manchester, England aliiambia BBC kuwa, lava katika Mlima Nyiragongo ni ya kimiminika na ina uwezekano wa kusonga haraka.

Picha iliyochukuliwa kwa ndege ikionesha uharibifu wa nyumba viungani mwa mji wa mji wa Goma.

Takriban watu 15 wamethibitishwa kufariki kutokana mlipuko wa volkano uliotokea katika Mlima wa Nyiragongo, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) lakini huenda idadi ya vifo ikaongezeka wakati maafisa wakiyafikia maeneo yaliyoathirika zaidi.

Volkano ililipuka katika mlima Nyiragongo una kumwaga ujiuji wa moto ama lava uliolifanya anga kuwa jekundu.

Ilibainika kuwa, Jumamosi iyopita, lakini lava hiyo haikuhfika katika mji wa Goma unaokaliwa na watu milioni mbili kusini mwa mlima huo.

Wakazi wa vijiji vya karibu na mlima huo pamoja na mji Goma ambao waliyakimbia makaazi yao kwa hofu ya mlipuko huo, wameanza kurejea huku wengi wao wakiwasaka jamaa zao waliopotea.

Watu tisa miongoni mwa waliothibitishwa kufariki dunia, walipoteza maisha katika ajali za barabarani, wakati watu walipokuwa wakihaha kukimbia ili kuokoa maisha yao.

Wanne walikufa walipokuwa wakijaribu kutoroka gerezani huku wawili wakiungua hadi kufa, alisema msemaji wa serikali Patrick Muyaya Jumapili.

Zaidi ya watoto 170 wanahofiwa kupotea na wengine 150 wametengana na familia zao, kulinga na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) ambalo linasema litaweka vituo vya kuwapokea watoto watakaopatikana wakiwa peke yao.

Lava iliishia karibu na wilaya ya Buhene, viungani mwa mji wa Goma na kuangamiza mamia ya nyumba na hata majengo makubwa.

Ukarabati unatarajiwa kuchukua miezi kadhaa, ambapo ilifahamika kuwa, nyumba zote zilizopo katika wilaya ya Buhene zimeungua,” Innocent Bahala Shamavu aliliambia shirika la habari la kimataifa la Associated Press.

Wakazi wamekuwa wakipekua kusaka mabaki katika nyumba zao zilizoangamizwa, huku Maafisa nchini Rwanda wamesema zaidi ya watu 3,000 wamevuka mpaka kutoka Goma.

Baadhi walianza kurejea Goma na wengine walikwenda kwenye maeneo ya milimani Magharibi mwa mji wa Goma.

Mkazi mmoja wa Goma Richard Bahati, alisema kuwa alikuwa ndani ya nyumba wakati aliposikia watu wakipiga mayowe, na akaingia wasiwasi mkubwa alipoona anga limegeuka kuwa jekundu nje.

Kwengineko, lava ilikatiza katika moja ya barabara kuu inayounganisha Goma na mji wa Beni, ambayo ni njia muhimu ya usambazaji wa misaada.

Hata hivyo, uwanja wa ndege wa wa mji wa Goma haukuguswa na lava, kinyume na ripoti za awali kwamba uliathiriwa.

Mitikisiko ilisikika baada ya kulipuka kwa volkano hiyo, alisema Bw Muyaya. “Watu wanashauriwa kuendelea kuwa macho, kuepuka safari zisizo za lazima, na kufuata maelekezo,” ulisema ujumbe wake wa Twitter.

Wakazi wa Goma walianza kuzikimbia nyumba zao kabla serikali kutangaza mpango wa namna ya kuondoka katika mji huo.

Umati wa watu ulionekana usiku ukiondoka kwa miguu huku baadhi yao wakiwa wamebeba magodoro na mali zao nyingine.

Mfanyabiasha mkazi wa Goma, Kambere Ombeni, alikuwa miongoni mwa wale waliorejea kwenye eneo la tukio wakati vifusi vya nyumba vilipokuwa bado vinafuka moshi.

“Tulitazama eneo lote linalozingira Nyiragongo likiungua na kufuka moshi, moto ulitoka hapa, hata sasa bado tunaona lava,” alisema.

Mkazi mwingine Irene Bauma, alisema watu watahitaji msaada kutoka serikalini kuyajenga upya maisha yao.

“Kuna ardhi, watu ambao wamepoteza kila kitu, labda pia kuna vifo, nani anayejua? tunaiomba serikali kuja na kuwasaidia manusura wa mlipuko huu ,”alieleza.

Tom Peyre-Costa, kutoka Baraza la Wakimbizi la Norway mjini Goma, Norwegian Refugee Council, aliiambia BBC jinsi tukio la mlipuko wa volcano lilivyotokea.

Mfanyabiasha mkazi wa Goma, Kambere Ombeni, alikuwa miongoni mwa wale waliorejea kwenye eneo la tukio wakati vifusi vya nyumba vilipokuwa bado vinafuka moshi.

“Tulitazama eneo lote linalozingira Nyiragongo likiungua na kufuka moshi, moto ulitoka hapa, hata sasa bado tunaona lava,” alisema.

Mkazi mwingine, Irene Bauma, alisema watu watahitaji msaada kutoka serikalini kuyajenga upya maisha yao.

“Kuna ardhi, watu ambao wamepoteza kila kitu, labda pia kuna vifo, nani anayejua? tunaiomba serikali kuja na kuwasaidia manusura wa mlipuko huu,”alieleza.

Tom Peyre-Costa, kutoka Baraza la Wakimbizi la Norway mjini Goma -Norwegian Refugee Council, aliiambia BBC jinsi tukio la mlipuko wa volcano lilivyotokea.