NA MWANDISHI WETU
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amefanya uteuzi wa Wakurugenzi katika Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliytiwa saini na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar, Injinia Zena Ahmed Said, uteuzi huo umeanza Mei 2, mwaka huu.
Katika uteuzi huo, Dk. Mwinyi alimteua Dk. Salum Soud Hamed kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Makame Omar Makame ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uhifadhi wa Maeneo ya Baharini, Dk. Zakaria Khamis kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Uvuvi wa Mazao Baharini na Capt. Hamad Bakari Hamadi, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maendeleo ya Uchumi wa Buluu.
Aidha dk. Mwinyi, alimteua Sheha Idrissa Hamdani kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Adam Abdulla Makame, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mamlaka ya Udhibiti (Utafutaji na Uchimbaji) wa Mafuta na Gesi Asilia, Zanzibar (ZPRA), Mikidad Ali Rashidi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia, Zanzibar (ZPDC) na Dk. Ameir Haidar Mshenga, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Uvuvi, Zanzibar (ZAFICO).